Posts

Showing posts from December, 2012

David Mangare: Yatima aliyethubutu

Image
Na Dismas Lyassa, Mwananchi   
Tajiri maarufu Duniani, Bill Gates wakati fulani amewahi kunukuliwa akisema kinachowasumbua watu wengi kutofanikiwa ni wao wenyewe kutopenda kuthubutu. Siku moja akiwa kwenye chuo kimoja akitoa nasaha zake, Bill Gates alisema “Mwanafunzi niliyesoma nae ambaye alikuwa akinishinda kwenye mitihani mingi, sasa hivi nimemuajiri, ni fundi wangu, alinishinda elimu darasani, mimi leo namshinda utajiri, amekuwa kati ya maelfu ya wafanyakazi ninaowalipa mshahara”.
Anachosema Bill Gates ni ukweli kuwa kusoma au kutosoma, ama kuzaliwa familia tajiri au maskini, sio tiketi kwamba unaweza kuwa tajiri au la.
Siri ya ushindi Kinachoweza kumsaidia mtu kuwa na maisha yenye mafanikio ni uwezo wake katika kuthubutu kufanya mambo, hasa pale anapoyafanya kwa ustadi huleta tija zaidi.
Mtafiti wa masuala ya saikolojia, Norman Vincent Peale wa Marekani anasema katika kitabu chake cha Maisha yenye Mafanikio kuwa kujiamini ni silaha nyingine muhimu kama kweli unataka kuwa mwenye mafanik…

Ndoa ni ninyi,siyo watu wa nje

Image
Ndoa ni ninyi wenyewe, Siyo watu wa nje
SIRI moja kubwa ya kuwa na ndoa nzuri ni wanandoa wenyewe kujitambua kuwa wao ndiyo wenye deni la kuimarisha uhusiano walionao.

Ndiyo kusema kuwa kila siku katika maisha yako, unapaswa kutafuta mbinu za kufanya ili uhusiano wenu uendelee kuwa mzuri.
Siku moja nilikuwa napita Sinza (Dar es Salaam), nikamsikia dada mmoja akijibizana na mwenzi wake kwenye simu; Aah! kwani wewe unataka muda huu niwe wapi? Haya basi niko chooni.

Hayakuwa majibu mazuri, kiasi dada mwingine aliyekuwa karibu, akamsihi mwenzake asizungumze vile.Watu wengi wanapenda kuwa na ndoa nzuri, lakini wao hawajui kuwafanyia mazuri wenzao. Utakuwaje na ndoa nzuri wakati kauli zako ni chafu?

Jitahidi kuwa na kauli nzuri kwa mwenzi wako. Hata pale mwenziyo anapokukosea, zungumza naye kwa njia ya kuondoa kasoro, si kutukanana. Siku zote waza namna ya kuujenga uhusiano wenu. Usidhani ndoa nzuri za wenzio ni jambo linaloshindikana kwako, hapana. Ndoa haijengwi kwa matofali, bali kauli n…

MSINGI WA MAISHA BORA NI KUFANYA KAZI KWA BIDII

Image
MSINGI WA MAISHA BORA NI KUFANYA KAZI KWA BIDIINa Dismas Lyassa
KWANINI katika maisha kuna watu wengine hawafanikiwa na wengine wanafanikiwa? Ni swali ambalo limekuwa likiumiza vichwa vya wengi.
Wapo ambao wanawianisha mafanikio ya mtu na elimu, lakini hiyo haina ukweli sana, japo kuna watu ambao mafanikio yao yametokana na elimu waliyonayo. Kusoma au kutosoma kwa maana ya kupata elimu ya kutosha siyo ile ya kufuta ujinga haina maana kwamba mtu atakuwa na maisha mazuri au atafanikiwa katika maisha au laa.
Tunasisitiza kuwa elimu ni muhimu sana katika masiaha ya sasa. Lakini hiyo unaitumia vipi hilo ndilo suala au jambo la msingi sana ambalo wengi wanashindwa kulitambua. Kutokana na kushindwa kujua hilo wengi huishia kutoa wasifu wa viwango vya elimu.
Aah! Unajua mimi nimesoma na Rais wenu… alikuwa kilaza sana, mara oooh usinione hivi nimesoma sana, nimetembelea nchi nyingi sana hapa duniani au aaah… nimeonana na wakubwa wengi katika dunia hii na mengine kama hayo. Kila mtu anapenda kufan…