Posts

Showing posts from January, 2017

Trump aagiza ukuta ujengwe kati ya Marekani na Mexico

RAIS wa Marekani Donald Trump ametia saini amri ya rais kuidhinisha kuanza kujengwa ukuta katika mpaka kati ya Marekani na Mexico. Amri hiyo inalenga kutimiza mojawapo ya ahadi kuu za Trump alizozitoa wakati wa kampeini.

Akizuru wizara ya mambo ya ndani hapo jana kutia saini maagizo mawili ya Rais, Trump amewaagiza maafisa nchini Marekani kuanza kazi ya kupanga na kuujenga ukuta huo mpakani akisema nchi isiyokuwa na mipaka sio nchi.

Tayari sehemu ya mpaka huo kati ya Marekani na Mexico ulikuwa umewekewa uzio lakini Trump amesema ukuta unahitajika kuwazuia wahamiaji haramu kutoka nchi hiyo ya Amerika ya kusini kuingia Marekani na pia kuagiza ukaguzi wa mipaka kukamilishwa katika kipindi cha siku 180 zijazo.
Mwaka jana, Trump alisema lengo la ukuta huo ni kuwazuia wahamiaji kutoka Mexico kuingia Marekani kwani huleta matatizo mengi yakiwemo dawa za kulevya, uhalifu na ubakaji. Amesisitiza kuwa gharama ya ukuta huo inayotarajiwa kuwa mabilioni ya dola itagharamiwa na Mex…