Posts

Showing posts from June, 2017

WATU 18 HOI NA MMOJA AFARIKI DUNIA KUTOKANA NA UGOJWA EWA KIPINDI PINDU

Na Baraka lusajo. Kalambo. UGONJWA wa kipindupindu umelipuka katika kijiji na kata ya Samazi katika Mwambao wa ziwa Tanganyika wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa na kusababisha kifo cha mtoto eliyefahamika kwa jina la lina Protas miaka 5 na wengine 18 wamelazwa kwenye zahanati ya kijiji hicho. Afisa tarafa ya Kasanga wilayani humo Peter Mankambila , alisema chanzo cha ugonjwa huo kimetokana na wavuvi waliokuwa wametokea katika kijiji cha Mpasa kilichopo wilaya jilani ya Nkas,ambao walifika kijijini hapo kwa shughuri za uvuvi na kuwambukiza wengine. Alisema kwa kawaida wavuvi huwa wanahama hutoka eneo moja kwenda eneo lingine , ambapo katika siku za hivi karibuni walipata taarifa ya uwepo wa ugonjwa huo katika kijiji cha Mpasa kilichopo katika wilaya jilani ya Nkasi, ambapo walitoa ushauri kwa wavuvi kuto elekea kwenye maeneo hayo. Alisema baada y…

Dkt. John Pombe Magufuli ziarani Pwani

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewahakikishia wananchi wa Pwani kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imejipanga kuhakikisha miradi mikubwa ya maendeleo yenye manufaa kwa mkoa huo na Taifa kwa ujumla inatekelezwa kama alivyoahidi. Mhe. Rais Magufuli amesema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Bwawani Mjini Kibaha akiwa katika siku ya kwanza ya ziara yake ya kikazi ya siku 3 Mkoani Pwani. Mhe. Dkt. Magufuli ameitaja miradi hiyo kuwa ni ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge) ambayo imeanza kujengwa, ujenzi wa barabara ya njia sita kati ya Dar es Salaam na Chalinze yenye urefu wa Kilometa 128, ujenzi wa bandari kavu ya Ruvu itakayopokea mizigo ya kutoka bandari ya Dar es Salaam na ujenzi wa mradi wa umeme katika maporomoko ya mto Rufiji (Stiegler’s Gorge) ambao mipango ya utekelezaji kwa kushirikiana na Ethiopia imeanza. Amebainisha kuwa pamoja na kutekeleza miradi hiyo Serikali ya Awamu ya Tano itaendelea …

BMT YABARIKI UCHAGUZI TFF, LATOA MAAGIZO

Baraza la Michezo Tanzania (BMT), limebariki Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) likisema: “Tunaitakia TFF uchaguzi mwema wenye amani, upendo na utulivu.” Pamoja na baraka hizo, Baraza limeiagiza TFF kuwaelekeza wagombea wote kuzipitia sheria za Baraza la Michezo, Kanuni za Baraza na kanuni za Usajili, hususani kanuni ya 8 (1) na (2). Kanuni hiyo ya 8 (1) na (2), inaagiza kuwa endapo wagombea wote watakaoshinda nafasi wanazowania kwa sasa ndani ya TFF, hawana budi kuachia nafasi mojawapo katika uongozi wa mpira kwa miguu katika ngazi ya wilaya au mkoa aliyoshinda awali. BMT imetoa agizo hilo ikiwa ni kukumbushana juu ya utii wa sheria na kuepuka kushika nyadhifa mbili kwa wakati mmoja. Katika barua yake iliyoandikwa Juni 19, mwaka huu na kusainiwa na Katibu Mkuu wa BMT, Mohammed Kiganja, Baraza hilo limesema: “Uchaguzi huu usivuruge amani iliyopo nchini. Wagombea wakumbuke kuwa kuna maisha baada ya uchaguzi.” Baraza limesisitiza kuwepo na haki katika …

Ndoa ni ninyi wenyewe, siyo watu wa nje

Na Dismas Lyassa SIRI moja kubwa ya kuwa na ndoa nzuri ni wanandoa wenyewe kujitambua kuwa wao ndiyo wenye deni la kuimarisha uhusiano walionao. Ndiyo kusema kuwa kila siku katika maisha yako, unapaswa kutafuta mbinu za kufanya ili uhusiano wenu uendelee kuwa mzuri. Siku moja nilikuwa napita Sinza (Dar es Salaam), nikamsikia dada mmoja akijibizana na mwenzi wake kwenye simu; “Aah kwani wewe unataka muda huu niwe wapi? Haya basi niko chooni.” Hayakuwa majibu mazuri, kiasi dada mwingine aliyekuwa karibu, akamsihi mwenzake asizungumze vile. Watu wengi wanapenda kuwa na ndoa nzuri, lakini wao hawajui kuwafanyia mazuri wenzao. Utakuwaje na ndoa nzuri wakati kauli zako ni chafu? Jitahidi kuwa na kauli nzuri kwa mwenzi wako. Hata pale mwenziyo anapokukosea, zungumza naye kwa njia ya kuondoa kasoro, si kutukanana. Siku zote waza namna ya kuujenga uhusiano wenu. Usidhani ndoa nzuri za wenzio ni jambo linaloshindikana kwako, hapana. Ndoa haijengwi kwa matofali, bali kauli njema na matendo…

WANAOTUHUMIWA WA MAUAJI YA KINYAMA IGUNGA WAFIKISHWA MAHAKAMANI

Na Allan Ntana, Igunga. WATU watatu akiwemo mganga wa kienyeji katika wilaya ya Igunga mkoani Tabora wamekamatwa na jeshi la polisi na kufikishwa katika mahakama ya hakimu mfawidhi wilayani Igunga kwa tuhuma ya mauaji ya mwanamke. Waliofikishwa mahakamani ni Juma Idd (25), Tatu Juma (20) wakazi wa kijiji cha Tambalale tarafa ya Simbo wilayani Igunga na Shida Mwanasimbila (54) ambaye ni mganga wa kienyeji mkazi wa kijiji cha Kipungulu kata ya Mzibamziba tarafa ya Puge wilaya ya Nzega. Akiwasomea shitaka mbele ya hakimu wa wilaya ya Igunga Ajali Milanzi mwendesha mashitaka wa jeshi la polisi Mengo Kamangala. Ameiambia mahakama kuwa mei 25, 2017 majira ya saa 5 usiku katika kijiji cha Tambalale tarafa ya Simbo wilayani hapa washitakiwa wote kwa pamoja walimuua kwa kumkata na kitu chenye ncha kali Elizabeth Charles (45) mkazi wa kijiji hicho cha Tambalale. Mwandesha mashitaka aliendelea kuiambia mahakama kuwa baada ya kufanya mauaji washitakiwa walikata kiganja cha mkono wa …

74 WACHUKUA FOMU, KUREJESHA TFF

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUNI 20, 2017 74 WACHUKUA FOMU, KUREJESHA TFF Wanafamilia 74 wa mpira wa miguu, wamechukua na kurejesha fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Agosti 12, mwaka huu. Hadi zoezi hilo linafungwa leo Juni 20, 2017 saa 10.00 jioni wagombea wote wamerejesha ambako kwenye nafasi ya urais, jumla ya wagombea 10 walijitokeza kuomba nafasi hiyo wakati kwenye makamu rais wamejitokeza sita. Wadau 58 wamejitokeza kuwania nafasi za ujumbe wa kamati ya utendaji katika Katika Kanda mbalimbali. Zoezi la kuchukua na kurejesha fomu kwa mujibu wa Kanuni ya 10, limefanyika kwa siku tano kuanzia Juni 16, 2017 hadi Juni 20, mwaka huu. Siku ya kwanza ilipoanza tu, Jamal Malinzi alikuwa wa kwanza kuchukua fomu na kurejesha huku akifuatiwa na Imani Madega, Wallace Karia, Fredrick Masolwa, Athumani Nyamlani, Fredrick Mwakalebela, John Kijumbe, Shija Richard, Ally Mayay na Emmanuel Kim…

Airtel yazindua vocha ya shilingi 200

Airtel yaleta TABASAMU, yazindua vocha ya shilingi 200 nchini · Airtel wazindua vocha ya kiwango cha chini kabisa kwa wateja wa simu za mkononi Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imezindua vocha mpya ya muda wa maongezi kwa wateja wake wa malipo ya awali nchini itakayowaongezea wateja wake TABASAMU pale wanapopiga simu au kuitumia kwa matumizi yoyote ya kuwasiliana au kujiunganisha kwenye vifurushi vya gharama nafuu. Vocha hiyo mpya ya TABASAMU kwa shilingi 200 inapatikana kwa wachuuzi wote wa vocha za Airtel na kuwawezesha wateja wa Airtel na watanzania wote watakaojiunga na Airtel kumudu gharama za mawasiliano wakati wowote kwa gharama nafuu zaidi Akiongea wakati wa uzinduzi, Meneja Masoko wa Airtel , Bi Aneth Muga alisema “ Leo tunajisikia fahari kuzindua na kuitambulisha sokoni vocha ya muda wa maongezi ya shilingi 200 itakayowapatia wateja Tabasamu na uhuru wa kuwasiliana na ndugu jamaa marafiki au wale wajasiliamali kuweza kuitumia kupanga mipango yao wak…

SERIKAL KUJA NA MKAKATI KUNUSURU MAUAJI

Na Steven Augustino, Tenduru SERIKALI imeahidi kutengeneza mkakati wa madhubuti wa kupambana na Wanyama wakali ili kuwalinda wananchi ambao wamekuwa wakiuawa na wengine kupata madhara kwa kupata vilema vya maisha. Kupitia taarifa hiyo pia imewataka wananchi ambao wamekuwa wakiishi katika maeneo yenye wanyama wakali kuwa na tahadhari wakati wote ili kuiokoa na madhara hao. Hayo yalisemwa na Mkuu wa wilaya ya Tunduru Jua Homera wakati akiongea na Wananchi na wafiwa katika mazishi ya Mkulima wa Kijiji cha Kajima kilichopo katika kata ya Kalulu Wilayani Tunduru aiyefahamki kwa jina la Mauwa Athuman Daud (43) aliye fariki dunia katika tukio la kushambuliwa na Tembo. Akifafanua taarifa hiyo Dc, Homera alisema kuwa kwa kuanzia tayali amekwisha andika andiko la namna ya madhara ambayo yamekuwa yakiwapata wananchi wanaoishi katika maeneo yenye Wanyama wakali pamoja na mikakati na kuiwasilisha Wizara husika kwa ajili ya utekelezaji. Awali akizungumzia tukio la mauaji hayo mume wa mar…
Image
PICHA NAMBA 1 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akizungumza na mkuu wa chuo cha ulinzi cha Taifa cha Rwanda Kamishina wa Polisi wa Rwanda Felix Namhoranye ofisini kwake makao makuu ya Jeshi la Polisi. Kamishina Namhoranye ni kiongozi wa msafara wa maafisa mbalimbali kutoka chuo cha ulinzi cha Taifa cha Rwanda ambao wapo nchini kwa ziara ya mafunzo. Picha na Hassan Mndeme – Jeshi la Polisi. Picha namba 2 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akizungumza na maofisa wa polisi kutoka nchi mbalimbali za Afrika mashariki na Afrika magharibi ambapo wanasoma chuo cha ulinzi cha Taifa cha Rwanda hawapo picha. Kushoto ni mkuu wa chuo cha ulinzi cha Taifa cha Rwanda, Kamishina Felix Namhoranye na kulia ni Kamishina wa Polisi Jamii , Mussa Alli Mussa – picha na Hassan Mndeme – Jeshi la Polisi. Picha namba 3 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa Polisi kutoka nchi mbalimbali wanaosoma chuo cha…

Sakata la Makinikia: Watanzania tuondoe hofu, tumuamini Rais wetu

Tangu uongozi wa Kampuni ya Barrick, ambayo ndio yenye hisa nyingi katika kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia iliyo katika mgogoro na Serikali kutangaza kuwa ipo tayari kutafuta mwafaka kwa njia ya mazungumzo, kumekuwepo na baadhi ya watanzania wanaonesha wasiwasi juu ya kufanikiwa kwa jambo hilo. Katika Makala hii Mwandishi Said Ameir wa Idara- Habari MAELEZO anasisitiza kuwa watanzania hawapaswi kuwa na wasi wasi hata chembe. Ni tangazo lililoleta faraja kwa watanzania wengi kwa kuwa wanaamimi kuwa hatua ya kufanya mazungumzo na ile kauli ya Mwenyekiti wa Barrick Profesa John Thornton kuwa wapo tayari kuilipa Tanzania kila kile kilichostahili ambacho kampuni ya Acacia haikuilipa, ni uamuzi mwafaka. Kwanza imani ya watanzania wengi imejengwa kutokana na uthabiti wa matokeo ya Kamati zote mbili; Kamati ya Kuchunguza Aina na Viwango v…

HabinderSeth Singh na Rugemarila wako kizimbani leo kwa kesi ya tuhuma ya uhujumu uchumi.

Image
HabinderSeth Singh na Rugemarila wako kizimbani leo kwa kesi ya tuhuma ya uhujumu uchumi.

WAUMINI WA KIISLAMU WATUMIE MWEZI WA RAMADHANI KUKEMEA UHARIFU

Na Mwandishi Wetu,Pwani WAUMINI wa dini ya kiislamu waliopo katika Kata ya Kongowe Halmashauri ya Mji wa Kibaha wametakiwa kuutumia mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa kutanguliza mbele maslahi ya nchi katika kuhubiri amani pamoja na kukemea vitendo vya uharifu vinavyofanywa na baadhi ya watu. Diwani wa kata ya Kongowe Idd Kanyalu(CCM),alitoa wito huo juzi wakati akizungumza na waumini zaidi ya 200 wa msikiti wa Bamba mara baada ya kumaliza zoezi la kufuturisha lililokuwa likifanyika msikitini hapo. Kanyalu,alisema kuwa mwezi wa Ramadhani ni mwezi ambao kila muumini anapaswa kuuheshimu kwa kutenda mambo mema yanayompendeza mwenyezi Mungu hivyo ni fursa nzuri ya kuhakikisha wanaleta mabadiliko katika jamii. Alisema, wapo watu wachache ambao wamekuwa wakifanya vitendo vya uharifu vinavyopelekea uvunjifu wa amani katika nchi yetu jambo ambalo haliwezi kukubalika kwa kuwaacha watu hao waendelee . Kanyalu,alisema kuwa ni wakati muafaka kwa waumini wote wa dini ya kiislamu kuhakikisha wanaut…

WANASHERIA WATAKA MFUMO WA SHERIA ZA KIMATAIFA ZA MADINI UCHUNGUZWE

Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO. Mtaalam mbobevu wa Sheria za Madini na Mafuta nchini, Dkt. Adelardus kilangi ametoa rai kwa wanasheria watakaoteuliwa kwa ajili ya kurekebisha Sheria za Madini kuanza kufanya kwanza uchunguzi katika Sheria za Kimataifa za Madini ili waweze kuishauri vizuri serikali. Rai hiyo imetolewa leo na mtaalam huyo katika mahojiano maalum na mwandishi wa habari hii kuhusu maoni juu ya ripoti ya uchunguzi wa mchanga wa madini iliyowasilishwa na baadhi ya wachumi pamoja na wanasheria walioteuliwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli. Dkt. Kilangi amesema kuwa ripoti iliyowasilishwa imeonesha madhaifu yaliyopo katika sekta ya madini ambayo madhaifu hayo yamegawanyika katika maeneo ya mfumo wa Sheria pamoja na mfumo wa usimamizi ambapo tatizo kubwa limekuwa ni kukosa uzalendo kwa viongozi waliopewa dhamana ya kufanya maamuzi ya nchi. “Katika eneo la mfumo wa Sheria, kwanza nampongeza Rais Magufuli kwa kuwataka wanasheria na wataalamu wengine kufanya mapitio ya Sheria…

MCHANGA WA DHAHABU: MSIMAMO WA MAGUFULI WAILAINISHA BARRICK

• Habari za Taarifa za Kamati za Kuchunguza Makinia zatawala ulimwengu • Bosi wa Barrick akubali yaishe Said Amer, Maelezo Kwa kipindi cha zaidi miezi 4 sasa suala la mchanga wa dhahabu au Makinikia limetawala vichwa vya habari vya vyombo vya habari vya ndani na nje. Katika Makala hii Mwandishi Said Ameir wa Idara ya Habari- MAELEZO anaeleza uzito wa habari kwa kuangalia mustakbala wa makampuni ya madini na mataifa yanayotoka. Ni dhahiri kuwa dunia hivi sasa inatafakari kuhusu namna ya kukabiliana na dharuba hii ya Rais Magufuli dhidi ya makampuni ya madini. Mabepari wa madini wamepatwa na kiwewe kwa sababu msimamo wa Rais Magufuli unawaamsha wengine waliolala nao kudai haki zao kama wanavyofanya watanzania. Kwa lugha za vijana wa kileo wanasema ‘JPM ameliangusha ‘Dude’ ambalo limeleta taharuki kubwa katika viota vya biashara ya madini- mfano majiji ya London, New York, Geneva, Otawa, Vancouver na kwengineko katika sekta nzima ya biashara ya madini ulimwenguni. Kwa karibu …

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan ajumuika na waumini wa dini ya Kiislamu

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amejumuika na waumini wa dini ya Kiislamu,wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam, viongozi mbalimbali wa Serikali na wa vyama vya siasa katika halfa ya futari aliyoiandaa katika makazi yake Oysterbay Jijini Dar es Salaam. Katika Hafla hiyo ya futari, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan alishiriki katika utoaji wa vyeti kwa wadau wa mazingira ambao walishiriki kikamilifu katika maadhimisho ya wiki ya Mazingira Duniani iliyofanyika Kitaifa tarehe 4-June-2017 - Butiama mkoani Mara. Baadhi ya taasisi zilizopatiwa vyeti na Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ni Shirika la Utangazaji Tanzania- TBC, Clouds Media, Lake Gas limited, Tbl, Zantas Air na WWF. Akizungumza kwa Niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan katika hafla hiyo ya futari, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira …

HARBINDER SIGHN SETH NA JAMES RUGEMALILA WA SAKATA LA ESCROW WAMEKAMATWA

Image
TAKUKURU inawashikilia HARBINDER SIGHN SETH NA JAMES RUGEMALILA ikiwatuhumu kwa makosa ya UHUJUMU UCHUMI

CCM Bunda yandaa maandamano ya amani

CHAMA cha Mapinduzi(CCM) Wilayani Bunda mkoani Mara, wameazimia kuandaa maandamano ya amani ikiwa ni hatua ya i kumuunga mkono Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa hatua alizochukua ya kupambana na upotevu wa madini ambayo yamesababishia taifa hasara. Hayo yalifikiwa katika kikao cha viongozi wa CCM wa matawi na kata za mji wa Bunda kilicho fanyika katika ofisi kuu ya chama hicho wilayani humo. Akifunga kikao hicho jana Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Bunda Chacha Gimanwa alisema, amekubali maandamano yafanyike tarehe na siku watakayoipanga na alisisitiza kuwa, chama cha mapinduzi kinamuumga mkono rais kwa mapambano dhidi ya wahujumu uchumi na rasilimali za nchi. Mwenyekiti wa CCM kata ya Balili, Bonifas Sungwa alisema ,anampongeza rais magufli kwa kuunda tume hiyo ambayo imefichua wizi wa kutisha wa mapato ya madini ambao unasababisha umasikini wa watanzania. Katibu mwenezi wa ccm wa Kata ya Nyasura Frank Mamba alikipongeza kikao hicho klichoitishwa na Mwenykiti wa CCM wila…

Tanzania kuunda kikosi kazi maalum kuhusu wafugaji

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amesema ataunda kikosi kazi maalum ambacho kitafanya kazi ya kuchunguza matatizo mbalimbali yanayowakuta wafugaji kote ili Serikali iweze kuwasaidia kutatua matatizo hayo ikiwemo kukosekana kwa maeneo rasmi yaliyotengwa rasmi kwa ajili ya malisho ya mifugo nchini. Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Viongozi wa Chama cha Wafugaji nchini ambao walimpelekea kilio chao kuhusu matatizo na manyanyaso wanayopata wakiwa katika shughuli zao za ufugaji Ikulu, Dar es Salaam. Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema amepokea mapendekezo ya wafugaji hao na Serikali itafanyia kazi ili kuondoa hali ya sintofahamu inayowakuta wafugaji katika maeneo mbalimbali nchini kwa sasa. Makamu wa Rais pia amewataka wafugaji waache kutumika kama mtaji wa kisiasa kwani kufanya hivyo kutarudisha nyuma jitihada za kuimarisha na kuboresha shughuli zao nchini. Amesema ili …

Wasomi, Wananchi Wapongeza Bajeti

Jovina Bujulu na Benjamin Sawe-MAELEZO BaadhiyawasominawananchiwameisifubajetiyaSerikalikwamwaka 2017/18wakisemakuwaimelengakumkomboamwananchinaimeakisi ahadi za Rais za kusaidia Tanzania ya uchumi wa viwanda. Akizungumzia bajeti hiyo, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Dk. BensonBanaamesemakuwabajetihiyoinajibumaswalimengiyaliyo kwenye Ilani ya Chama Cha Mapinduzina Mpango wa Maendeleo ya Miaka Mitano2020/21 na Dira ya Taifaya Mwaka 2020/25 na kwamba ni yenye kutegua vitendawili vinavyowakabili wananchi katika kujiletea maendeleo. ‘’Kwasurayabajetiilivyonibajetiyenyeukombozikwamwananchiwa kawaidakwasababuinagusamasualayakupunguziwakodikwenye pembejeo,vyakula,kilimo,miundombinu,umemenamaji’’,amesemaDk Bana. Naye Dk Bashir Ally ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ameipongeza bajeti hiyo na kushauri kuwa baada ya kupitishwa, mchakato wa utekelezaji uanze kwa hamasa ya kisiasa, kitaaluma na kijamii ili ku6kia malengo yake. ‘’Unaweza kuwa na mpango mzuri, lakini ikiwa watekelezaji …

Bunda watoa ya moyoni kuhusu Bulaya na Bunge, wapambana na polisi kuzuia msafara wa Samia

Na Mwandishi wetu, Bunda.
SIKU  chache  baada ya  kamati ya maadili  ya Bunge la jamhuri  wa Muungano  wa Tanzania,  kuwapa adhabu  wabunge  wawili , Esta Bulaya (jimbo la Bunda mjini) na Halima Mdee( jimbo  la Kawe) kwa  kuwafungia   kuhudhuria  vikao vitatu  vya Bunge  hadi  bunge la bajeti  mwakani baadhi  ya  wazee jimbo la Bunda mjini  wameibuka  na kudai hawakutendewa haki  wananchi  wa majimbo hayo.
Wazee  hao  wakizungumza  na waandishi  wa habari  jana  walisema adhabu hiyo  ya kukaa nje  ya bunge  kwa kipindi  cha miezi  10  ni kubwa mno  na haiendani  na kosa  walilotenda  Bulaya  na Mdee  badala yake  ni kuwaadhibu  wananchi  wa majimbo  hayo  kwa kuwakosesha uwakilishi  bungeni  kwa kipindi  chote  hicho.
“Sisi  wanabunda  tunasema,  hawajamuadhibu  Bulaya,  bali wametuadhibu  sisi  wanabunda  tuliomchagua, na tunadhani  hii sio haki,  ni uvunjifu  wa kidemokrasia,  tunamuomba  Spika wa Bunge, mheshimiwa  Ndugai  kuangalia  kwa makini jambo hili  anapoliongoza bung…