SERIKAL KUJA NA MKAKATI KUNUSURU MAUAJI


Na Steven Augustino, Tenduru SERIKALI imeahidi kutengeneza mkakati wa madhubuti wa kupambana na Wanyama wakali ili kuwalinda wananchi ambao wamekuwa wakiuawa na wengine kupata madhara kwa kupata vilema vya maisha. Kupitia taarifa hiyo pia imewataka wananchi ambao wamekuwa wakiishi katika maeneo yenye wanyama wakali kuwa na tahadhari wakati wote ili kuiokoa na madhara hao. Hayo yalisemwa na Mkuu wa wilaya ya Tunduru Jua Homera wakati akiongea na Wananchi na wafiwa katika mazishi ya Mkulima wa Kijiji cha Kajima kilichopo katika kata ya Kalulu Wilayani Tunduru aiyefahamki kwa jina la Mauwa Athuman Daud (43) aliye fariki dunia katika tukio la kushambuliwa na Tembo. Akifafanua taarifa hiyo Dc, Homera alisema kuwa kwa kuanzia tayali amekwisha andika andiko la namna ya madhara ambayo yamekuwa yakiwapata wananchi wanaoishi katika maeneo yenye Wanyama wakali pamoja na mikakati na kuiwasilisha Wizara husika kwa ajili ya utekelezaji. Awali akizungumzia tukio la mauaji hayo mume wa marehemu Mauwa, Bw. Said Kalolo alisema kuwa chanzo cha tukio hilo ni marehemu kuwamulika tembo hao kwa kutumia tochi jambo ambalo lilionesha kuwakera ha hivyo kumshamulia na kufariki dunia papo hapo. Alisema kuwa tukio hilo lilitokea Juni 17 majira ya saa 4 usiku baada ya kundi la tembo hao kumvamia wakati akiwa anawafukuza watoke shambani kwake. Aidha katika taarifa hiyo Kalolo pia aliwatupia lawama maafisa wa idara ya mani hai wanaolinda wanyama katika kituo cha uhifadhi wa wanyama pori Kalulu kilichopo katika hifadhi ya taifa ya Selous kuwafukuza tembo hao katika maeneo waliyo kuwepo. Akizungumzia tukio hilo kwa njia ya simu Kaimu afisa Wanyama pori wa Wilaya hiyo Limbega Alli pamoja na kudhibitisha kuwepo kwa tukio hilo alisema kuwa tayali yeye kwa kushirikiana na askari wa kitengo hicho wapo katika eneo la tukio na tayari wameanza kuwafukuza tembo hao ili wasiendelee kuleta madhara kwa wananchi. "ni kweli tukio hilo lipo ila kwa sasa mimi na kikosi nchangu tunashiriki zoezi la kuwafukuza Tembo hao tukiwa tunashirikiana na maafisa wa kikosi cha uhifadhi cha kalulu pamoja na askari wa askari wa Jumuiya ya ulinzi shirikishi wa wanayama pori wa Vijiji (VGS) Nalika kuwafukuza tembo hao " alisema Limbega. Alisema hilo ni tukio la nne kwa wanyama kusababisha vifo kwa wananchi ambapo kati yake matukio mawili yalisababishwa na wanyama aina ya Fisi na mawili yamesababishwa na wanyama pori aina ya Tembo. Mganga aliye ufanyia uchunguaizi mwili wa marehemu Athuman Dkt. Goerg Chiwangu alisema kuwa chanzo cha kifo hicho kilisababishwa na kutokwa na damu nyingi kwa ghafula. Alisena katika tukio hilo marehemu aliumia vibaya kichani, kifuani, alitobolewa Tumboni, pamoja na kuvunjwa vunjwa miguu na mikono yote pamoja na pondwa pondwa na kusababisha viungo vya ndani kusagika kabisa.

Comments

Tanzania

TAARIFA MBAYA KWA WAVUTAJI WA SIGARA, TUMBAKU

HOTUBA YA WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO, MHE. UMMY A. MWALIMU (MB), KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2018/2019

MADAI YA WAFANYAKAZI YASABABISHA VIFAA VYA UJENZI VYA KAMPUNI YA  CEYTUN KUZUIWA UWANJA WA NDEGE TABORA.