WANAOTUHUMIWA WA MAUAJI YA KINYAMA IGUNGA WAFIKISHWA MAHAKAMANI


Na Allan Ntana, Igunga. WATU watatu akiwemo mganga wa kienyeji katika wilaya ya Igunga mkoani Tabora wamekamatwa na jeshi la polisi na kufikishwa katika mahakama ya hakimu mfawidhi wilayani Igunga kwa tuhuma ya mauaji ya mwanamke. Waliofikishwa mahakamani ni Juma Idd (25), Tatu Juma (20) wakazi wa kijiji cha Tambalale tarafa ya Simbo wilayani Igunga na Shida Mwanasimbila (54) ambaye ni mganga wa kienyeji mkazi wa kijiji cha Kipungulu kata ya Mzibamziba tarafa ya Puge wilaya ya Nzega. Akiwasomea shitaka mbele ya hakimu wa wilaya ya Igunga Ajali Milanzi mwendesha mashitaka wa jeshi la polisi Mengo Kamangala. Ameiambia mahakama kuwa mei 25, 2017 majira ya saa 5 usiku katika kijiji cha Tambalale tarafa ya Simbo wilayani hapa washitakiwa wote kwa pamoja walimuua kwa kumkata na kitu chenye ncha kali Elizabeth Charles (45) mkazi wa kijiji hicho cha Tambalale. Mwandesha mashitaka aliendelea kuiambia mahakama kuwa baada ya kufanya mauaji washitakiwa walikata kiganja cha mkono wa kulia na kuondoka nacho kusikojulikana. Alisema washitakiwa wote kwa pamoja walitenda kosa hilo kinyume na kifungu 196 kanuni ya adhabu sura ya 16 mapitio ya 2002 inayozuia kutenda makosa kama hayo. Hata hivyo washitakiwa hawakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza shauri hilo ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi juni 23 mwezi huu itakapotajwa tena na washitakiwa wamepelekwa gerezani. Mwisho.

Comments

Tanzania

TAARIFA MBAYA KWA WAVUTAJI WA SIGARA, TUMBAKU

HOTUBA YA WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO, MHE. UMMY A. MWALIMU (MB), KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2018/2019

MADAI YA WAFANYAKAZI YASABABISHA VIFAA VYA UJENZI VYA KAMPUNI YA  CEYTUN KUZUIWA UWANJA WA NDEGE TABORA.