WATU 18 HOI NA MMOJA AFARIKI DUNIA KUTOKANA NA UGOJWA EWA KIPINDI PINDU


Na Baraka lusajo. Kalambo. UGONJWA wa kipindupindu umelipuka katika kijiji na kata ya Samazi katika Mwambao wa ziwa Tanganyika wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa na kusababisha kifo cha mtoto eliyefahamika kwa jina la lina Protas miaka 5 na wengine 18 wamelazwa kwenye zahanati ya kijiji hicho. Afisa tarafa ya Kasanga wilayani humo Peter Mankambila , alisema chanzo cha ugonjwa huo kimetokana na wavuvi waliokuwa wametokea katika kijiji cha Mpasa kilichopo wilaya jilani ya Nkas,ambao walifika kijijini hapo kwa shughuri za uvuvi na kuwambukiza wengine. Alisema kwa kawaida wavuvi huwa wanahama hutoka eneo moja kwenda eneo lingine , ambapo katika siku za hivi karibuni walipata taarifa ya uwepo wa ugonjwa huo katika kijiji cha Mpasa kilichopo katika wilaya jilani ya Nkasi, ambapo walitoa ushauri kwa wavuvi kuto elekea kwenye maeneo hayo. Alisema baada ya muda kupita wavuvi wa tarafa hiyo walidaiwa kuelekea kwenye maeneo hayo , ambapo inadaiwa waliupata ugonjwa huo na kuwambukiza wengine. ‘’tuligundua uwepo wa ugonjwa huo kwenye kijiji cha Samazi baada ya baadhi ya wananchi kuugua na kulazwa kwenye zahanati ya kijiji hicho , ambapo mpaka sasa umesababisha kifo cha mtoto mwenye umri wa miaka mitano ambae alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu kwenye zahanati hiyo’’alisema Mankambila. Alisema kufikia sasa watu 18 wamelazwa na wanaendelea na matibabu na kusema licha ya hilo timu ya wilaya hiyo imefika kwenye kijiji hicho na kuanza kutoa elimu kwa wananchi juu na namna ya kuepukana na ugonjwa huo hatari. Alisema wametoa elimu kwenye maeneo ya vjijiji tofauti ikiwemo kijiji cha kipwa, kasanga, kipanga , kisala na samazi , na kusema wamejikita zaidi kwenye maeneo hayo kutokana na vijiji hivyo kuwa mpakani na ziwa hilo. Mtendaji wa kata hiyo , Tedsoni Chonya , alisema baada ya kujitokeza kwa ugonjwa huo walitoa taarifa kwenye uongozi wa wilaya na kwenye idara ya afya , ambapo viongozi wote walifika na kujionea adha hiyo kisha kutoa elimu kwa wananchi. Alisema kwa kuwa wataramu wa afya wamekwisha kufika wanaimani ugonjwa huo utaisha kwa haraka na kuwa chanazo nikutokana na wananchi wa kijiji hicho kwenda kijiji cha mpasa ambako ndiko waliupatia. Aidha chonya alisema licha hiyo pia wavuvi kwenye maeneo hayo wamekuwa wakitumia maji ya ziwa Tanganyika bila kuchemsha na hivyo kuwa na wasiwasi kuwa huenda ikawa ndio chanzo cha kujitokeza kwa ugonjwa huo. Afisa afya wilaya humo , Andondile Mwakilima ambae licha ya kukili wazi kuwepo adha hiyo alisema mpaka sasa watu (8) wameruhusiwa kurudi nyumbani na watu 8 wanaendelea kupatiwa matibabu kwenye zahanati hiyo. Mkuu wa wilaya hiyo Julith Bunyura , alisema ili kutokomeza ugon jwa huo wananchi wanakila sababu ya kutumia maji safi na salama sambamba na kichimba vyoo vya kudumu. Alisema licha ya hilo wanaendelea kutoa elimu kuzunguka kwenye vijiji na kata tofauti ili kutoa elimu dhidi ya kuepukana na ugonjwa huo.

Comments

Tanzania

TAARIFA MBAYA KWA WAVUTAJI WA SIGARA, TUMBAKU

HOTUBA YA WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO, MHE. UMMY A. MWALIMU (MB), KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2018/2019

MADAI YA WAFANYAKAZI YASABABISHA VIFAA VYA UJENZI VYA KAMPUNI YA  CEYTUN KUZUIWA UWANJA WA NDEGE TABORA.