Posts

Showing posts from July, 2017

Ravi Zacharias says the World Is Watching

Image
The world is looking for relevance in the Christian gospel. What better way to show this than how we live our lives, centered around Christ, his cross, and compassion? Ravi Zacharias draws from Acts 24 to demonstrate the crucial need for Christians to communicate the gospel not only through their words, but through their actions.

Msiwaonee haya viongozi wasiojali maendeleo, CCM waambiwa

Image
Na Dismas Lyassa WANACHAMA wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wametakiwa kutowaonea haya viongozi ambao wanaonekana kutokuwa mstari wa mbele kushirikiana na wananchi katika kuharakisha maendeleo nchini. Kauli hiyo imetolewa jana na Mwenyekiti wa Wanawake wa CCM Wilaya ya Kibaha Mjini, Mwanid Kiongoli akifungua rasmi mkutano uliokuwa na lengo la kuchagua viongozi wa wanawake katika Kata ya Pangani, wilayani Kibaha Mjini, Mkoa wa Pwani. “Rais wetu anataka maendeleo, mnamuona anavyofanya, anavyotembelea mikoa mbalimbali kusisitiza maendeleo, sisi tunatakiwa kumuunga mkono. Tumekuwa tukiona namna anavyowashughulikia wale ambao wanaonekana kutokwenda sawa na jitihada zake, hana mzaha, tunapaswa kwenda sambasamba na kasi hiyohiyo,” alisisitiza mwenyekiti huyo. Aidha aliwataka wananchi na wanachama kwa ujumla kutomuonea haya kiongozi au mtu yeyote ambaye kwa namna moja ama nyingine amepewa dhamana ndani au nje ya chama kuongoza chama au Serikali lakini hafanyi jitihada katika kuharakisha maende…

UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO WAJADILIWA

Na.Mwandishi Wetu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua ameongoza kikao cha Makatibu Wakuu cha Kujadili na kuupitisha Mwongozo wa Uratibu wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto nchini. Kikao hicho kilichofanyika Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma Julai 27, 2017 ambapo kilihusisha Makatibu wakuu pamoja na wadau wa maendeleo kwa lengo la kujadili mwongozo huo ili kuhakikisha utekelezaji wake unaanza mapema iwezekanavyo. Akizungumza wakati wa kikao hicho Dkt. Mwinyimvua alieleza umuhimu wa mwongozo ikiwa ni nyenzo muhimu ya kusaidia kutatua changamoto zinazowakabili wanawake na watoto ambapo kabla ya kuandaliwa Mwongozo huo, Tanzania ilikuwa na mipango kazi minane (8) ya kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na watoto.   “Lengo la Mwongozo huu ni kupunguza masuala ya ukatili kwa watoto na wanawake hivyo ni vyema ukajadiliwa na kuanza utekelezaji wake mapema ili kutatua changamoto za wanawake na watoto katika jamii.”Alisema D…

MAKAMU WA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA MBOWE WILAYA YA HAI ATIMKIA CCM

Image
Makamu wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro ajiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) Katika hali isiyotarajiwa kwenye medani za siasa Mkoa wa Kilimanjaro na kipekee katika Wilaya ya Hai, leo tarehe 26 Julai 2017, Makamu wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai na Diwani wa Kata ya Machame Magharibi (Chadema) Ndugu Goodluck A. Kimaro ametangaza kuachana na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Pamoja na ndugu Kimaro, madiwani wengine wawili ndugu Evarist Kimathi Diwani wa Kata ya Mnadani na ndg. Abdalah Chiwili Diwani wa Kata ya Weruweru wameachia ngazi na uanachama kutoka Chadema. Katika Mkutano na waandishi wa habari ulioitwa na Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kilimanjaro na kuhudhuriwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro Ndg. Iddi Juma, Katibu wa CCM Mkoa wa Kilimajaro Ndg. Jonathan Mabihya na viongozi wengine wa Chama kutoka Mkoa wa Kilimanjaro. Mgeni Rasmi katika shughuli hiyo ya kuwapokea viongozi hao wa Chadema alikuwa Ndg. H. …

Dk. Kigwangalla akabidhi gari la wagonjwa jimboni kwake

Image
Mbunge wa jimbo la Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla amekabidhi gari maalum la kubebea wagonjwa (Ambulance) mpya na la kisasa katika Kituo cha Afya Busondo kilichopo Tarafa ya Puge ambalo litakuwa msaada mkubwa kwa wananchi wa Nzega Vijijini. Tukio hilo la kukabidhi gari hilo limefanywa na Mkuu wa Wilaya ya Nzega, mkoani  Tabora, Mh. Geofrey Ngupula ambaye alitoa agizo kali kwa Mganga Mkuu wa Kituo hicho kuhakikisha gari hilo linatumika kwa shughuli zilizokusudiwa ikiwemo za kubebea wagonjwa na akina mama wajawazito kuwawaisha sehemu muhimu za kutolea huduma stahiki. Mkuu wa Wilaya huyo alimpongeza Mbunge wa Jimbo hilo Dk. Kigwangalla kwa kuweza kuwasaidia wananchi  wa Jimbo hilo kwa kuweza kuwasaidia gari hilo la Wagonjwa  kwani litasaidia kuokoa maisha ya wananchi hao ambao wapo maeneo ya mbali na kituo cha Afya huku pia likitarajiwa kuwa msaada kwa kuwapeleka wateja katika  ngazi za juu za …

Maghembe: waandishi saidieni kuwafichua majangili

Na Yusuph Mussa, Tanga WAZIRI wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe amewataka waandishi wa habari kuwafichua kwa kutumia kalamu zao watu wanaojihusisha na ujangili. Amesema pamoja na jitihada zinazofanywa na Serikali za kupambana na ujangili, bado majangili wapo, na wengine ndani ya Shirika la Hifadhi la Taifa (TANAPA), hivyo waandishi wakitumia mbinu zao watafanikisha. Aliyasema hayo jana (Julai 27) wakati anafungua warsha ya siku tatu kwa wahariri na waandishi wa habari waandamizi nchini unaofanyika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga. "Ujangili bado ni tatizo kubwa, lakini tunashukuru mmeweza kulielezea mpaka watu wameweza kuogopa. Lakini bado tunataka muingie kwenye vita hii. Sio kwa kutumia bunduki, bali kalamu zenu. "Tunataka ile kauli ya Rais (Dkt. John Magufuli) itimie kuwa majangili wakiona tembo wawakimbie, lakini sio tembo kuwakimbia binadamu. Ni ukweli, kwa sasa mauaji kwa tembo wetu yamepungua, na majuzi tumeona mizoga ya tembo wawili Hifadhi…

DC  ATOWA AGIZO LA KUKAMATWA  KWA MWALIMU MKUU NA WAZAZI WATATU WA WANAUNZI WALIOPATA MIMBA

Na George Mwigulu, Nkasi   SERIKALI wilayani Nkasi mkoani Rukwa imeliagiza jeshi la polisi wilayani humo kumkamata mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mwai , Mashaka Aderson  na wazazi wa watoto watatu waliokatiza  masomo baada ya kupata ujauzito  ili sheria ichukue mkondo wake.   Mkuu wa wilaya hiyo Said Mtanda alimuagiza mkuu wa Polisi Wilaya ya Nkasi ,(OCD) David Mtasya  ili kumkamata mwalimu huyo mkuu pamoja na wazazi hao ambao wanaonesha wanakwamisha jitihada za serikali katika suala zima la kupambana na suala la wanafunzi kupata ujauzito.   Watoto hao watatu walimepata ujauzito  wakiwa wanasoma darasa la Tano katikaShule ya Msingi Mwai  iliyopo katika Kata ya Mtenga wilayani Nkasi katika mkoa wa Rukwa . Mtanda alisema kuwa amelazimika kutoa agizo hilo kwa OCD baada ya kubainika kuwepo kwa mpango  kati ya Mwalimu Mkuu ,Anderson  na wazazi wa watoto  hao kumaliza shauri hilo kwa usiri mkubwa pasipo kufikisha katika vyombo vya sheria. Aidha mkuu huyo wa polisi wa wilaya ya taya…

IMANI POTOFU ZIMEDAIWA KUCHANGIA VIFO VYA AKINAMAMA NA WATOTO

Na  Patrick Mabula , Kahama. Julai 27 , 2017.   Imani potofu, uelewa mdogo  na ukosefu wa elimu  juu ya  magonjwa ya binadamu  miongoni mwa jamii  ni miongoni mwa  chanzo  kinachochangia  vifo  vingi  vya akinamama na watoto wadogo wilayani  Kahama.   Hayo yameelezwa  juzi na kaimu mganga mkuu wa Halmashauri ya mji wa Kahama, Robart Rwebangila alipokuwa akiongea na waandishi wa habari na kusema  kutokuwa na uelewa , imani potofu na elimu kuhusu magonjwa ya  mbalimbali ya binadami     kunachangia  vifo vingi vya  watu hasa akinamama na watoto miongoni mwa jamii.   Rwebangila  alisema tatizo  hilo  limekuwa zikipelekea   vifo  hivyo  miongoni mwa jamii  kwa sababu mtu  anapougua wamekuwa hawaendi  hospitari   mapema  kuchunguza afya zao  na kupata matibabu  hadi  wanapokuwa  katika hali mbaya  kunakopelekea   watu  kupoteza  maisha.   Alisema kunachangamoto  kubwa  miongoni mwa jamii  ya  imani potofu, uelewa  mdogo   na ukosefu wa elimu  kuhusu  magonjwa ya binadamu  na kusababisha  …

Wanzania 96 Wanufaika na Ufadhili wa Masomo Uholanzi

Na. Georgina Misama - MAELEZO Watanzania 96 kutoka Serikalini, sekta binafsi na asasi za kiraia, wamenufaika na ufadhili wa masomo kutoka seriklai ya Uholanzi ikiwa ni sehemu ya mpango wa Serikali hiyo kuchangia maendeleo nchini. Akiongea katika ghafla fupi ya kuwaaga Watanzania hao, iliyofanyika jana katika ukumbi wa Ubalozi wa Ufaransa Jijini Dar es Salaam, Balonzi wa Uholanzi nchini Tanzania Mhe.  Jaap Frederiks alisema kwamba Serikali ya Uholanzi kwa muda mrefu imekuwa ikichangia miradi ya maendeleo nchini Tanzania. Balozi Jaap alieleza kuwa Watanzaia waliofaidika na mpango huo unaojulikana kama Netherlands Fellowship Programme – NFP, ni waajiriwa kutoka Serikalini, sekta binafsi, wafanyabiashara wadogo pamoja na waajiriwa kutoka Asasi za kirai. “Kwa muda mrefu Tanzania imekuwa moja kati ya wafaidika wakubwa wa ufadhili wa Masomo Nchini Uholanzi program inayojulikana kama “Netherlands Fellowship Programme – NFP” ambapo zaidi ya Watanzania 5000 wamefaidika na ufadhili huo kati…

Elimu kwa Umma Yasaidia Kupunguza Uvamizi wa Ardhi

Na. Jacquiline Mrisho – MAELEZO Elimu kwa Umma inayotolewa na Serikali pamoja na Mashirika binafsi imesaidia kupunguza migogoro na uvamizi wa ardhi katika maeneo mbalimbali yaliyotengwa kwa ajili ya shughuli maalum. Hayo yamebainishwa hivi karibuni mkoani Morogoro na Afisa ardhi mteule Wilaya ya Mvomero, Keneth Mwenda wakati wa mkutano mkuu wa Kijiji cha Melela kilichopo wilayani humo, uliokuwa ukipitisha Mpango wa Matumizi ya Ardhi unaotekelezwa na Shirika la PELUM Tanzania. Mwenda alisema kuwa Bajeti Kuu ya Serikali peke yake haitoshelezi kutekeleza miradi yote hivyo amewashkuru wadau wa mashirika yasiyo ya kiserikali kwa kujitolea kushirikiana na Serikali kuwaletea wananchi maendeleo. “Serikali kuu pekee haiwezi kutekeleza mradi wa matumizi ya ardhi kwa vijiji vyote vya wilaya ya Mvomero, ndio maana tunatambua mchango mkubwa unaofanywa na shirika la PELUM Tanzania kuhakikisha vijiji vitano vya wilaya ya Mvomero vinapimwa na kupewa hati miliki,” alisema Mwenda. Vile vile ki…

Asilimia 53 ya Watanzania Wasema Usalama Umeimarika Nchini- Twaweza

Na Agness Moshi na Jonas Kamaleki- MAELEZO Zaidi ya nusu ya Watanzania wamesema kuwa hali ya usalama nchini imeimarika  ikilinganishwa na miaka takriban miwili iliyopita na kuwafanya wananchi waishi kwa utulivu na amani. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika lisilo la Kiserikali lijulikanalo kama Twaweza, Bw. Aidan Eyakuze wakati akiwasilisha matokeo utafiti wa “Hapa Usalama Tu: Usalama, Polisi na Haki nchini Tanzania” kupitia sauti za wananchi kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam. Bw. Eyakuze alisema kuwa takwimu zilizo kusanywa na sauti za wananchi kwa mwaka huu zimeonesha kuimarika kwa usalama kwa wananchi wa Tanzania Bara ikilinganishwa na miaka iliyopita. “Tumeongea na watu 1805 kuwauliza hali ya usalama katika maeneo wanayoishi na asilimia 53 ambayo ni sawa na nusu ya Watanzania Bara wamesema hali ya usalama imeimarika na inaridhisha” alisema Bw.Eyakuze. Bw.Eyakuze amesisitiza kuwa wamekusanya taarifa kutoka kwa wananchi wenyewe,  kupitia simu zao …

Raila Odinga awataka Wakenya wasifanye 'mchezo wa baba na mama wanapigana' mkesha wa uchaguzi

Image
Raila Odinga awataka Wakenya wasifanye 'mchezo wa baba na mama wanapigana' mkesha wa uchaguzi Mgombea wa urais katika muungano wa NASA nchini Kenya Raila Odinga Mgombea wa urais katika muungano wa NASA nchini Kenya Raila Odinga amewataka wafuasi wake kutoshiriki tendo la ndoa mkesha wa siku ya uchaguzi. Bwana Odinga amefananisha uchaguzi huo na vita akisema kuwa kushiriki ngono kabla ya kwenda vitani ni mkosi mbaya ambao unaweza kusababisha mtu kushindwa. ''Tunaenda vitani na lazima tuhifadhi nguvu yetu kabla ya siku ya vita ambayo ni Agosti 8'', alisema mjini Homabay eneo la magh ahribi mwa Kenya. ''Hakuna hata mmoja wetu ambaye anafaa kushiriki ngono kabla ya mkesha wa siku ya uchaguzi'. Odinga hususan aliwasisitizia wanaume akisema itasababisha wengine wao kutopiga kura. Wanawake alisema ,hawafai kukubali kushiriki katika tendo la ndoa na waume zao usiku wa kuamkia siku ya uchaguzi, alisema. ''Kila mwanamke anafaa kumnyima mumewe haki…

SERIKALI HAIJAFUTA MAFUNZO KWA WATUMISHI WA UMMA

SERIKALI HAIJAFUTA MAFUNZO KWA WATUMISHI WA UMMA Serikali haijafuta mafunzo kwa watumishi wa umma ambapo Taasisi za Serikali zimeelekezwa kuandaa Mpango wa Mafunzo kwa watumishi kwa njia ya uwazi na shirikishi ili kuepuka malalamiko kutoka kwa baadhi ya watumishi wa umma. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) amesema hayo leo katika kikao kazi na Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, jijini Dar es Salaam. Mhe. Kairuki amesema mwajiri anapoandaa Mpango wa Mafunzo kwa watumishi wake ni vyema mpango huo ukawa shirikisha kwa watumishi wote ili kujua mpangilio wake, ikiwa ni pamoja na kuandaa orodha ya ziada ya watumishi watakaochukua nafasi za wale waliopangwa kushiriki mafunzo lakini wakashindwa. “Napokea malalamiko mengi sana kuhusiana na upendeleo katika suala la mafunzo, napenda kuwasisitiza waajiri tuandae Mpango wa Mafunzo ambao ni shirikishi kwa watumishi wote kuepuka haya, wengine wan…

MASALIA YA MIJUSI MIKUBWA KUTORUDISHWA NCHINI

Na Octavian Kimario-WHUSM Dodoma WAZO la kuwarudisha nchini Dinosaria halina tija kutokana na ugumu wa Kiteknolojia na gharama ikilinganishwa na faida za kuchukua hatua hiyo. Akijibu swali la Mbunge wa Mchinga, Hamidu Hassan Bobali lililo uliza,Ni nini kauli ya mwisho ya Serikali kuhusu faida ambayo wananchi wa Lindi na Tanzania kwa ujumla wananufaika kutokana na mabaki hayo. Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Ramo Makani amesema Tanzania itaendelea kusisitiza kupata manufaa kutokana na uwepo wa Dinosaria wake huko Berlin-Ujererumani. “Kufuatia majadiliano ya kina yaliyohusisha wataalamu wabobezi katika masuala ya Malikale kutoka pande zote mbili imekubalika kuwa Serikali ya Ujerumani itaendesha shughuli za utafiti zaidi huko Tendaguru na katika maeneo jirani ili kuwezesha uchimbaji wa mabaki ya Dinosaria wengine yanayoaminika kuwepo katika maeneo hayo pamoja na kuanzisha Kituo cha Makumbusho ili shughuli za Utalii zifanyike katika eneo hilo na kuvutia watalii kutoka nchini …

Taarifa njema kwa wanaotaka kusoma nje

Karibu Global Source Watch (GSW), tunaviwakilisha vyuo zaidi ya 78 vya Marekani, Canada, India, Malaysia, China nk... Baadhi ya vyuo vya nje gharama zake ni za chini zaidi kuliko vyuo vya Tanzania...kwa mfano hiki... wasiliana nasi tukuunganishe moja kwa moja kupitia email:globalsourcewatch@gmail.com ******************** Shilingi moja ya Tanzania ni sawa na Sh1.6 ya Uganda; fedha yetu ina thamani zaidi ya yao... 2017 TUITION & FEES STRUCTURE Cavendish University has revised its rules with regards to payment and registration. We encourage all students to familiarize themselves with these rules for their own benefit. Click Here to read the Student Payment and Registration Policy Program Name Duration Day Evening Weekend Distance Learning Masters' Degrees Master Of Science In Public Health 2 Years 2,017,000 Master Of Business Administration 2 Years 1,917,000 1,271,500 Master Of Business Administration - Accounting & Finance 2 Years 1,917,000 1,271,500 Master Of Business …

BUNGE KUPOKEA TAARIFA YA MIKATABA YA RASILIMALI ZA TAIFA.

MWANDISHI WA AZAM TV APOTEA...

Image
Una taarifa zozote kuhusu Fatna Ramole? @fatnaramole Mfanyakazi mwenzetu @azamtvtz hajulikani alipo. Unaweza kutoa taarifa zake kwa namba hii 0719669749 Asante. @ Dar es Salaam, Tanzania taarifa hii ni kwa mujibu Raymond Nyamwihula

AUWAWA KIKATILI KWA KUCHOMWA KISU

MTU mmoja anayefahamika kwa jina la Adam Joseph(30) ameuawa kwa kuchomwa kisu na mpwa wake anayejulikana kwa jina la Benjamin Zakaria miaka(22) kwa madai kuwa ni hasira za kumdai gunia moja la alizeti. Tukio la mauaji limetokea usiku wa kuamkia Jana majira ya saa 3 baada ya mpwa wake huyo kumfuata mjomba wake kilabuni na kisha kuanza kumdai gunia hilo la alizeti. Akizungumza na gazeti hili Afisa mtendaji wa kijiji cha Ninga wilayani Kalambo mkoani Rukwa Yohana Kawea alisema kuwa baada ya watu hao kuwa wanadaiana gunia hilo la alizeti alimfuata kilabuni na kisu na kisha kumchoma na kumuua hapo hapo. Alisema kuwa baada ya kumuua alifanikiwa kutoroka na kukimbilia kusiko julikana ambapo polisi wanamtafuta kufuatia tukio hilo. Katika tukio jingine Geofrey Richard (8) mkazi wa kijiji cha Mvuna mandakelenge wilayani Nkasi mkoani Rukwa amekufa baada ya kupigwa na kitu chenye ncha kali kichwani na mtu anayedhaniwa kuwa ni mlevi. Mtoto huyo akiwa na wenzie Juni 29 mwaka h…

WAANDISHI WA HABARI WAJERUHIWA AJALI SINGIDA

Na Waandishi wetu Watu tisa wakiwemo Wanahabari wa watatu wanafunzi na mtoto mdogo wamejeruhiwa baada ya gari waliyokuwa wakisafiria kupinduka katika Kijiji cha Mkenge barabara ya Singida Ilongero Mtinko Halmashauri ya Wilaya ya Singida. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida ACP Debora Magiligimba ameeleza kuwa ajali hiyo ilitokea juzi saa 11:40 jioni ambayo ilihusisha gari la abiria T 972 BPV aina ya Noah lililotoka Mtinko kuelekea mjini Singida lilipoacha njia na kupinduka wakati dereva wake akijaribu kulipita gari lililokuwa mbele yake. Magiligimba aliwataja majeruhi hao ambao ni wanahabari akiwemo Elisante Mkumbo (49) wa ITV, aliyepata maumivu shingoni, Doris Megji (39) wa AZAM TV alijeruhiwa mkono wa kulia na Ismal Abdala mpiga picha wa kujitegemea aliyeumia shingoni na kifuani wote wakazi wa Halmashauri ya Manispaa ya Singida. “Waandishi hao ambao walikuwa wakielekea mjini Singida kuwahi kutuma taarifa za Mwenge kwenye vyombo vyao, Walikimbizwa kwenye Hospitali ya Mkoa huo wal…

JPM Awaonya Wanasiasa Wanaotetea Wahalifu

Image
Na Mwandishi Wetu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Magufuli ameawaonya baadhi ya Wanasiasa kuacha mara moja tabia ya kuwatetea watu wanaoshikiliwa na vyombo vya usalama kwa tuhuma za kujihusisha na uhalifu. Rais Magufuli ametoa onyo hilo leo Jijini Dar es Salaam wakati akiweka jiwe la msingi la mradi wa uboreshaji wa bandari ya Dar es Salaam. “Kuna mwanasiasa anazungumza kuwa hawa watu wamekaa sana lokapu (mahabusu) waachiwe wakati hawa watu wanahusika na mambo ya ajabu katika nchi. Kuna watu wamekufa kule zaidi ya 35, maaskari zaidi ya 15 na wanaohusika ni pamoja na hao lakini mtu anatoka anazungumza kwamba wamekaa mno. Unaweza ukaona ‘by implication’ kwamba huyu lazima anahusika kwa njia moja au nyingine”, alionya Rais. Amewataka wanasiasa wa namna hiyo kujifunza kunyamaza wakati serikali inafanya kazi yake. Aidha Rais Magufuli alieleza kusikitishwa na mmoja wa wanasiasa ambaye kimsingi hajawahi kusimama hata siku moja kulaani mauaji ya watu wasio na hat…

SERIKALI KUWAUNGANISHA WAZALISHAJI WAKUBWA WA CHAKULA KATIKA KATA TANO WILAYANI IRAMBA.

Serikali imedhamiria kuwaunganisha wakulima wakubwa wa mazao ya chakula wa kata tano za Wilaya ya Iramba kwa kujenga daraja na makaravati manne katika barabara yenye urefu wa kilomita 38.6 yatakayo gharimu shilingi bilioni 4.1. Akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa daraja la Mto Mtoa na makaravati katika barabara ya shelui-Mtoa-Urughu Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Amour Hamad Amour amesema serikali imedhamiria kuwaunganisha wananchi ili wazalishe mazao, waanzishe viwanda kisha kusafirisha bidhaa. Amour amesema kwakuwa barabara hiyo inahudumia wananchi wa kata za Shelui, Mtoa, Mtekente, Urughu na Ndago wananchi wa maeneo hayo watumie fursa ya kuwa na barabara nzuri kwa kutengeneza viwanda vidogo, vya kati na vikubwa na kisha kusafirisha bidhaa na sio mazao kama mali ghafi. Amesema kwa kufanya hivyo wakulima wa mazao wataweza kujiongeza kipato chao kwa kuwa hawatapunjwa kwa kuuzwa mali ghafi ambayo hupelekwa kwenye viwanda vya nchi nyingine hivyo barabara hiyo iwe hamasa kwao…