AUWAWA KIKATILI KWA KUCHOMWA KISU


MTU mmoja anayefahamika kwa jina la Adam Joseph(30) ameuawa kwa kuchomwa kisu na mpwa wake anayejulikana kwa jina la Benjamin Zakaria miaka(22) kwa madai kuwa ni hasira za kumdai gunia moja la alizeti. Tukio la mauaji limetokea usiku wa kuamkia Jana majira ya saa 3 baada ya mpwa wake huyo kumfuata mjomba wake kilabuni na kisha kuanza kumdai gunia hilo la alizeti. Akizungumza na gazeti hili Afisa mtendaji wa kijiji cha Ninga wilayani Kalambo mkoani Rukwa Yohana Kawea alisema kuwa baada ya watu hao kuwa wanadaiana gunia hilo la alizeti alimfuata kilabuni na kisu na kisha kumchoma na kumuua hapo hapo. Alisema kuwa baada ya kumuua alifanikiwa kutoroka na kukimbilia kusiko julikana ambapo polisi wanamtafuta kufuatia tukio hilo. Katika tukio jingine Geofrey Richard (8) mkazi wa kijiji cha Mvuna mandakelenge wilayani Nkasi mkoani Rukwa amekufa baada ya kupigwa na kitu chenye ncha kali kichwani na mtu anayedhaniwa kuwa ni mlevi. Mtoto huyo akiwa na wenzie Juni 29 mwaka huu majira ya saa 12 jioni alipigwa na mlevi huyo baada ya kuzomewa na watoto hao alipokuwa akipita barabarani kutokana na kulewa kupita kiasi. Taarifa iliyotolewa na kamanda wa polisi mkoani Rukwa George Simba Kyando ni kuwa baada ya mlevi huyo kuzomewa na watoto hao ndipo mlevi huyo alipopata hasira na kuamua kurusha kitu kizito chenye ncha kali kwa watoto hao na kuweza kumkuta mtoto huyo. Alisema kuwa mtoto huyo alipata majeraha makubwa kichwani na kukimbizwa katika kituo cha afya kirando kwa matibabu na muda mfupi mtoto huyo alifariki dunia. Kamanda Kyando alidai kuwa uchunguzi wa kitabibu ulibaini kuwa chanzo kikubwa cha kifo hicho ni kupasuka kwa fuvu na damu kuvujia kwenye ubongo. Mwili wa marehemu ulikabidhiwa kwa ndugu na kuendelea na shughuli nyingine za mazishi. Mtuhumiwa wa mauaji hayo anashikiliwa na jeshi hilo na pindi uchunguzi utakapokamilika atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.

Comments

Tanzania

TAARIFA MBAYA KWA WAVUTAJI WA SIGARA, TUMBAKU

HOTUBA YA WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO, MHE. UMMY A. MWALIMU (MB), KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2018/2019

MADAI YA WAFANYAKAZI YASABABISHA VIFAA VYA UJENZI VYA KAMPUNI YA  CEYTUN KUZUIWA UWANJA WA NDEGE TABORA.