DC  ATOWA AGIZO LA KUKAMATWA  KWA MWALIMU MKUU NA WAZAZI WATATU WA WANAUNZI WALIOPATA MIMBA


Na George Mwigulu, Nkasi   SERIKALI wilayani Nkasi mkoani Rukwa imeliagiza jeshi la polisi wilayani humo kumkamata mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mwai , Mashaka Aderson  na wazazi wa watoto watatu waliokatiza  masomo baada ya kupata ujauzito  ili sheria ichukue mkondo wake.   Mkuu wa wilaya hiyo Said Mtanda alimuagiza mkuu wa Polisi Wilaya ya Nkasi ,(OCD) David Mtasya  ili kumkamata mwalimu huyo mkuu pamoja na wazazi hao ambao wanaonesha wanakwamisha jitihada za serikali katika suala zima la kupambana na suala la wanafunzi kupata ujauzito.   Watoto hao watatu walimepata ujauzito  wakiwa wanasoma darasa la Tano katikaShule ya Msingi Mwai  iliyopo katika Kata ya Mtenga wilayani Nkasi katika mkoa wa Rukwa . Mtanda alisema kuwa amelazimika kutoa agizo hilo kwa OCD baada ya kubainika kuwepo kwa mpango  kati ya Mwalimu Mkuu ,Anderson  na wazazi wa watoto  hao kumaliza shauri hilo kwa usiri mkubwa pasipo kufikisha katika vyombo vya sheria. Aidha mkuu huyo wa polisi wa wilaya ya tayari amekwisha tekeleza agizo hilo ambapo pia kasi alilieleza gazeti hili  kuwa katika kukabiliana suala hilo amewakamata pia maofisa watendaji wa Kata wapatao sita wakituhumiwa  kushirikiana na wazazi kumaliza kesi za mimba shuleni kwa siri. Akizungumzia  tatizo hilo Mtanda amesema kuwa katika wilaya ya Nkasi tatizo hilo ni kubwa  ambapo sasa umekuwa kama mtindo ambapo watendaji wa kata , walimu wakuu wa shule  na wazazi wanashirikiana  kumaliza mashauri hayo kwa siri ili watoto hao waweze kuozeshwa kwa mahari ya fedha nyingi pamoja na ng'ombe.  “Kuanzia sasa  kwa kuwa orodha ya watuhumiwa hao tunayo  tutaanza mara moja  katika vyombo vya habari" alisema   " kwa wale ambao  wametoroka Serikali inatoa motisha  ili wasakwe na kufikishwa katika vyombo vya dola Hatuwezi kamwe kuendelea na mtindo huu wa ovyo wa kuwavumilia watu wanaofanya vitendo vya namna hii “ alisisitiza.   Mtanda alibainisha hayo wakati alipokuwa akihutubia kikao maalumu cha baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya hiyo ambacho kilikuwa kikijadili hoja ya Mkaguzi na Mdhibiti   wa Mahesabu  ya Serikali (CAG ) ambapo halmashauri hiyo  imepata hati safi

Comments

Tanzania

TAARIFA MBAYA KWA WAVUTAJI WA SIGARA, TUMBAKU

HOTUBA YA WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO, MHE. UMMY A. MWALIMU (MB), KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2018/2019

MADAI YA WAFANYAKAZI YASABABISHA VIFAA VYA UJENZI VYA KAMPUNI YA  CEYTUN KUZUIWA UWANJA WA NDEGE TABORA.