IMANI POTOFU ZIMEDAIWA KUCHANGIA VIFO VYA AKINAMAMA NA WATOTO


Na  Patrick Mabula , Kahama. Julai 27 , 2017.   Imani potofu, uelewa mdogo  na ukosefu wa elimu  juu ya  magonjwa ya binadamu  miongoni mwa jamii  ni miongoni mwa  chanzo  kinachochangia  vifo  vingi  vya akinamama na watoto wadogo wilayani  Kahama.   Hayo yameelezwa  juzi na kaimu mganga mkuu wa Halmashauri ya mji wa Kahama, Robart Rwebangila alipokuwa akiongea na waandishi wa habari na kusema  kutokuwa na uelewa , imani potofu na elimu kuhusu magonjwa ya  mbalimbali ya binadami     kunachangia  vifo vingi vya  watu hasa akinamama na watoto miongoni mwa jamii.   Rwebangila  alisema tatizo  hilo  limekuwa zikipelekea   vifo  hivyo  miongoni mwa jamii  kwa sababu mtu  anapougua wamekuwa hawaendi  hospitari   mapema  kuchunguza afya zao  na kupata matibabu  hadi  wanapokuwa  katika hali mbaya  kunakopelekea   watu  kupoteza  maisha.   Alisema kunachangamoto  kubwa  miongoni mwa jamii  ya  imani potofu, uelewa  mdogo   na ukosefu wa elimu  kuhusu  magonjwa ya binadamu  na kusababisha  watu  kupoteza maisha  hasa akinamama na watoto  wadogo kwa sababu wamekuwa wakichelewa kufika  hospitari  tayari ugonjwa ukiwa katika hatua mbaya .   Rwebangila alisema katika  mambo ya imani  kwa jamii yamekuwa katika  pande mbili  za mila na destuli ,  pamoja na imani ya  dini  kwa wagonjwa wanaugua na kkwenda kuombewa kwa viongozi wa madhehe  ya dini  kwa uponyaji.   Kaimu mganga mkuu huyo  ametowa wito kwa viongozi wa madhehbu ya dini  wanapowaombea wagonjwa kwenye  nyumba zao za ibada  kuwa  wanawaludisha  hospitari na vituo vya afya kufanyiwa vipimo  kama ugonjwa  umekwisha  na  kweli wamepona .   Rwebangira ametoa wito kwa jamii kuwa tabia ya kuwahi hospitari na vituo vya afya  kufanya vipimo  pale wanapojihisi kuwa na tatizo kwenye afya ya miili yao ili kuepuka gharama kubwa ya matibabu wanapochelewa  kufika hapo na kujikuta mgonjwa akiwa kwenye hali mbaya inayopelekea kifo.

Comments

Tanzania

HOTUBA YA WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO, MHE. UMMY A. MWALIMU (MB), KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2018/2019

Hatua za Ugonjwa wa UKIMWI

MAITI YAOKOTWA IKIWA KWENYE MFUKO, MIKONO NA MIGUU YAFUNGWA KAMBA KWA NYUMA