Raila Odinga awataka Wakenya wasifanye 'mchezo wa baba na mama wanapigana' mkesha wa uchaguzi


Raila Odinga awataka Wakenya wasifanye 'mchezo wa baba na mama wanapigana' mkesha wa uchaguzi Mgombea wa urais katika muungano wa NASA nchini Kenya Raila Odinga Mgombea wa urais katika muungano wa NASA nchini Kenya Raila Odinga amewataka wafuasi wake kutoshiriki tendo la ndoa mkesha wa siku ya uchaguzi. Bwana Odinga amefananisha uchaguzi huo na vita akisema kuwa kushiriki ngono kabla ya kwenda vitani ni mkosi mbaya ambao unaweza kusababisha mtu kushindwa. ''Tunaenda vitani na lazima tuhifadhi nguvu yetu kabla ya siku ya vita ambayo ni Agosti 8'', alisema mjini Homabay eneo la magh
ahribi mwa Kenya. ''Hakuna hata mmoja wetu ambaye anafaa kushiriki ngono kabla ya mkesha wa siku ya uchaguzi'. Odinga hususan aliwasisitizia wanaume akisema itasababisha wengine wao kutopiga kura. Wanawake alisema ,hawafai kukubali kushiriki katika tendo la ndoa na waume zao usiku wa kuamkia siku ya uchaguzi, alisema. ''Kila mwanamke anafaa kumnyima mumewe haki yake ya tendo la ndoa'' ,alisema. Raila awaomba wafuasi wake kutoshiriki ngono mkesha wa uchaguzi ''Hatua hiyo itatufanya kuamka mapema alfajiri ili kupiga kura na kulinda kura na kuilinda siku nzima hadi pale kura zitahesabiwa na kutangazwa'. Sio mara ya kwanza kwa kiongozi huyo wa chama cha ODM kukataza tendo la ngono wakati wa uchaguzi. Wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni za muungano wa NASA mjini Kakamega magharibi mwa Kenya , tarehe 3 mwezi Juni, Odinga aliwaambia wafuasi wake kusubiri hadi pale matokeo yatakapotangazwa ili kuweza kufurahia tendo hilo la ndoa. ''Nawaomba wanawake, kuwaambia waume zao kusubiri hadi baada ya uchaguzi ili kuweza kushiriki tendo hilo ili kusherehekea ushindi wetu''. Mshirikishe mwenzako Unavyoweza kumshirikisha mwenzako

Comments

Tanzania

TAARIFA MBAYA KWA WAVUTAJI WA SIGARA, TUMBAKU

HOTUBA YA WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO, MHE. UMMY A. MWALIMU (MB), KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2018/2019

MADAI YA WAFANYAKAZI YASABABISHA VIFAA VYA UJENZI VYA KAMPUNI YA  CEYTUN KUZUIWA UWANJA WA NDEGE TABORA.