WAANDISHI WA HABARI WAJERUHIWA AJALI SINGIDA


Na Waandishi wetu Watu tisa wakiwemo Wanahabari wa watatu wanafunzi na mtoto mdogo wamejeruhiwa baada ya gari waliyokuwa wakisafiria kupinduka katika Kijiji cha Mkenge barabara ya Singida Ilongero Mtinko Halmashauri ya Wilaya ya Singida. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida ACP Debora Magiligimba ameeleza kuwa ajali hiyo ilitokea juzi saa 11:40 jioni ambayo ilihusisha gari la abiria T 972 BPV aina ya Noah lililotoka Mtinko kuelekea mjini Singida lilipoacha njia na kupinduka wakati dereva wake akijaribu kulipita gari lililokuwa mbele yake. Magiligimba aliwataja majeruhi hao ambao ni wanahabari akiwemo Elisante Mkumbo (49) wa ITV, aliyepata maumivu shingoni, Doris Megji (39) wa AZAM TV alijeruhiwa mkono wa kulia na Ismal Abdala mpiga picha wa kujitegemea aliyeumia shingoni na kifuani wote wakazi wa Halmashauri ya Manispaa ya Singida. “Waandishi hao ambao walikuwa wakielekea mjini Singida kuwahi kutuma taarifa za Mwenge kwenye vyombo vyao, Walikimbizwa kwenye Hospitali ya Mkoa huo walipata matibabu na kuruhusiwa wao walitibiwa na kuruhusiwa, isipokuwa Doris Magji ambaye alilazwa na kuruhusiwa jana mchana wote wanaendelea vizuri “ Alisema Kamanda Magiligimba. Alielezea kuwa majeruhi wengine ni ambao walijeruhiwa sehemu mbalimbali za miili yao ambao ni Onesmo Daudi (16), Ombeni Daudi (12) na Joyce Daudi (14) ambao wote ni watoto wa familia moja wakiwa shule ya Sekondari ya Utemini Mjini Singida, Neema Rashidi (38), Maria Emmanuel (7) wakazi wa Mjini hapa. Majeruhi hao wamepelekwa Hospitali ya Misheni ya Mtinko, wakati jina la mtoto mdogo halikujulikana mara moja ambao wote hali zao zinaendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu. Alibaini kuwwa chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva wa gari hilo Boniface Kibauri (25) ambaye alikimbia baada ya ajali hiyo, aliyejaribu kulipita kushoto kwake gari lililomtangulia akiwa na mwendo kasi, hali iliyosababisha kuacha njia na kupinduka. “Tumempata mmiliki wa gari hilo lililopata ajali khafla Daniel Muro kwa ajili ya mahojiano kwa mujibu wa sheria za usalama Barabarani na kumtaka apeleke alete kumbukumbu za Dereva huyo ilikuwepo liseni na mkataba wake wa kazi ili kusaidia harakati za kumnasa na kumfikisha mbele ya sheria. Katika hatua nyingine majeruhi wakiwemo Wanahabari walidai kuwa walimshauri Dereva Boniface Kibauri kutolipita gari la mbele yake kwa kuwa ilikuwa ni Kinyume cha sheria, lakini hakufanya hivyo, na baada ya kupata nafasi gali lake lilichotwa na kupinduka mara tatu akisababisha abiria kujeruhiwa. Hata hivyo walilishauri jeshi la Polisi kuimarisha zaidi usalama kutokana na madereva wa vyombo vya moto kuendeshwa kiholela wakiwa kwenye barabara za vijijini, pamoja na serikali ya Mkoani humo kutoa magari maalum ya Wanahabari katika shughuli au misafara mikubwa Viongozi wakuu pamoja na Mwenge wa Uhuru, ili wafanye kazi zao vizuri bila usumbufu. Mwisho.

Comments

Tanzania

TAARIFA MBAYA KWA WAVUTAJI WA SIGARA, TUMBAKU

HOTUBA YA WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO, MHE. UMMY A. MWALIMU (MB), KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2018/2019

MADAI YA WAFANYAKAZI YASABABISHA VIFAA VYA UJENZI VYA KAMPUNI YA  CEYTUN KUZUIWA UWANJA WA NDEGE TABORA.