Jaffo akerwa 8 8 kugenuzwa 7 7


NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mkoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jaffo ameonesha kukerwa na vitendo vinavyofanywa na baadhi ya watu wanaobadilisha maana ya maadhimisho ya nane nane na kuwa maadhimisho ya sabasaba. Hatua hiyo inatokana na baadhi ya wananchi kutotambua kuwa maonyesho ya nane nane ni kwa ajili ya kilimo, ufugaji na uvuvi na si sehemu ya kufanyia biashara kama vile mabeseni pamoja na nguo huku wengine wakidaiwa kufika katika eneo hilo kwa lengo la kusikiliza muziki. Jaffo alieleza hayo wakati wa kilele cha maadhimisho ya nane nane kanda ya kati yaliyofanyika katika viwanja nane nane nzuguni na kusema kuwa hali hiyo inapelekea wananchi wengi kutofika katika maeneo hayo kwa lengo la kujifunza maswala ya kulimo. “Watu wanakuja kununua nguo,mabeseni ya kuwaogeshea watoto pamoja na nguo, wengine wanakuja kusikiliza mziki na vitu hivyo ambavyo wanakuja kununu vinapatikana saba saba hapa nane nane si mahali pake”alisema Jaffo. Alisema ili kuhakikisha kuwa heshima ya nane nane inafanikiwa kwa kiwango kinachotakiwa ni lazima kila mkurugenzi wa halmashauri za mikoa ya Dodoma na Singida kuweka mtu mmoja ambaye eneo lake la kazi litakuwa ni nane nane. “Mfano mkurugenzi wa Wilaya ya Mpwapwa unamleta mfanyakazi wako mmoja unamwambia yeye kijiji chake cha kufanyia kazi kinakuwa nane nane dodoma, ili kufanya maonyesho hayo kuwa ya kila siku na si ya msimu. “Maonyesho hayo yakiwa ya kila siku yatasaidi kuwafanya wakulima kutembelea kila siku kupata elimu ya kilimo, ufugaji na uvuvi, pia itasaidia maeneo haya kuwa active kutofauti na ilivyokuwa wiki chache zilizopita”alisema Jaffo. Alisema kuwa yote hayo yakitekelezwa ni wazi kuwa maonyesho ya nane nane yatafikiwa ya kiwango cha juu tofauti na ilivyo kwa sasa. Hata hivyo Jaffo alizielekeza halmashauri zote nchini kuhakikisha kuwa vituo vilivyotengwa kwa ajili ya kilimo vinafanya kazi kwa mwaka mzima. Alisema licha ya kuwa serikali imeweka vifaa vya kisasa pamoja na wataalam katika vituo hivyo lakini vituo hivyo vimekuwa vikitumika kwa msimu. “Tumeweka zana nyingi katika vituo hivyo, Computer,wataalamu kwa ajili ya kutoa elimu pamoja na vipeperushi lakini ukipita kwenye vituo hivyo unakuta havitumiki. “Kupitia ofisi za wakurugenzi wahakikisema vituo hivyo vinafanya kazi mwaka mzima, lengo ni wakulima wa eneo hili kufika na kupata elimu ya kilimu ili kuongeza tija katika kilimo”alisema. Kwa upande wake Naibu waziri wa kilimo, mifugo na uvuvi William Ole Nasha alisema kuwa wizara hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali kama vile mabadiliko ya tabia nchi ambayo kwa kiasi kikubwa inachangia kupungua kwa uzalishaji wa jita wa mazao na uhaba wa malisho ya mifugo. “Licha ya changamoto hizo lakini wizara kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo imeandaa na kuzindua muongozo wa kilimo unaohimili mabadiliko ya tabia nchi, na muongozo wa uzalishaji wa mazao kulingana na kanda za kilimo na kiekolojia. Alisema kuwa miongozo hiyo imeanza kusambazwa kwa wadau mbalimbali ikiwemo mamlaka za serikali za mitaa kwa ajili ya kutumia na maafisa ugani na wadau mbalimbali. Mwisho.

Comments

Tanzania

HOTUBA YA WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO, MHE. UMMY A. MWALIMU (MB), KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2018/2019

Hatua za Ugonjwa wa UKIMWI

MAITI YAOKOTWA IKIWA KWENYE MFUKO, MIKONO NA MIGUU YAFUNGWA KAMBA KWA NYUMA