KATIBU MKUU SIHABA NKINGA AHIMIZA KAZI ZA KUJITOLEA KATIKA KUTEKELEZA SHUGHULI ZA MAENDELEO MKOANI IRINGA.


DC SIKONGE AFUTA MABARAZA YA ARDHI YASIYOTENDEA HAKI WANANCHI Na Allan Ntana, Sikonge MKUU wa wilaya ya Sikonge Mkoani Tabora Peresi Magiri amepiga marufuku Mabaraza ya Ardhi ya Kata yanayoshindwa kutekeleza wajibu wake ipasavyo na kutotenda haki kwa wananchi katika usuluhishi wa migogoro ya ardhi. Magiri ametoa onyo hilo katika kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya hiyo kilichoketi katika ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi (FDC) wilayani humo. Alisema baadhi ya mabaraza utendaji wake hauridhishi kwa kuwa yamekuwa yakipindisha haki na kuchochea migogoro zaidi miongoni mwa walalamikaji hali inayopelekea kuongezeka kwa chuki na uhasama baina ya wahusika wanaohitaji kusuluhishwa. Alibainisha kasoro kubwa iliyoko katika mabaraza hayo kuwa ni wajumbe kukosa sifa za kufanya kazi hiyo jambo linawakosesha weledi na kutumia nafasi zao vibaya kwa kuendekeza masilahi binafsi katika utendaji wao. ‘Kuanzia leo Mabaraza yote yenye wajumbe wasio na sifa na yale ambayo yamekuwa yakilalamikiwa kwa kutotenda haki na yenye wajumbe waliomaliza muda wao ni marufuku kufanya kazi hiyo’, alisema. Alifafanua kuwa mabaraza yenye wajumbe wapya yanaruhusiwa kuendelea na kazi zao na yale ya zamani ambayo hayana matatizo na yanazingatia kanuni na taratibu za usuluhishi wa migogoro ya ardhi na hayajalalamikiwa yanaruhusiwa kuendelea ila akayataka kutenda haki vinginevyo atayapiga marufuku pia. Aliwataka Wenyeviti wa Serikali za Mitaa, Watendaji na Madiwani kumletea taarifa za mabaraza yote yanayolalamikiwa kwa kupindisha haki za wananchi na ambayo muda wake umeisha ili wahusika wachukuliwe hatua mara moja. Katika kuunga mkono uamuzi huo, Mbunge wa Jimbo la Sikonge Joseph Kakunda alitaka mabaraza yote yafanyiwe tathmini ili yale yenye wajumbe wasio na sifa waondolewe haraka ikiwemo kufanya tathmini ya sifa za wajumbe hao na uundwaji wake kama hauko sawa hatua zichukuliwa pia. Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo Simon Ngatunga aliunga mkono hatua hiyo na kuajidi kulifanyia kazi huku akiwataka wajumbe wote wa mabaraza hayo kutenda haki kwa wananchi ili kwenda na kasi ya serikali ya awamu ya tano ambayo inajali haki za wanyonge. Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Peter Nzalalila alionya watendaji na wataalamu wa halmashauri hiyo wanaoendekeza uzembe katika utendaji wao kwa kushindwa kufuatilia ufanisi wa miradi inayotekelezwa katika maeneo mbalimbali licha ya kutengewa fedha za kutosha.

Comments

Tanzania

TAARIFA MBAYA KWA WAVUTAJI WA SIGARA, TUMBAKU

HOTUBA YA WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO, MHE. UMMY A. MWALIMU (MB), KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2018/2019

MADAI YA WAFANYAKAZI YASABABISHA VIFAA VYA UJENZI VYA KAMPUNI YA  CEYTUN KUZUIWA UWANJA WA NDEGE TABORA.