MKUU WA MKOA AAGIZA BAKWATA KUPATIWA ENEO LAO


Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ameagiza halmashauri ya wilaya ya Karatu,kukabidhi Baraza kuu la waislamu nchini,Bakwata wilaya ya Karatu kiwanja chao kilichopo kata ya Karatu, kwa ajili ya kukimiliki na kukiendeleza .  Mkuu wa mkoa alitoa agizo hilo,kwenye kikao cha kusikiliza kero za ardhi wilayani humo kilichofanyika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa wilaya. Mkuu wa mkoa ameiagiza Halmashauri kutekeleza hukumu ya mahakama ya wilaya ya Karatu ambayo katika uamuzi wake iliamuru Bakwata kukabidhiwa kiwanja hicho  na kuwaondoa  ndugu watatu waliopo ndani ya kiwanja hicho kwa kuwafidia viwanja viwili kila mmoja eneo la njia panda ambalo walipewa awali na kulikataa. Amesema kuwa anashangazwa na kigugumizi cha halmashauri kushindwa kutekeleza uamuzi wa mahakama ambayo iliipatia Bakwata ushindi kwenye kesi iliyofunguliwa na ndugu watatu wakiongozwa na Erro Barani ambao walikaidi kuondoka kwenye eneo hilo kama walivyoamuriwa na mahakama. ’’Halmashauri mulipaswa kwenda mahakamani ili kuomba kibali cha kuwaondoa hao  ambao walishindwa kwenye kesi lakini hadi leo kimya jambo hili ni jepesi lakini watendaji wa halmashauri mnalifanya liwe gumu sielewi ni kwa nini’’aliuliza gambo. Amewataka watumishi wa Idara ya ardhi mkoani humo kusoma alama za nyakati waache ubinafsi  na tamaa na kuwaonya kuwa iwapo wasipobadilika wataharibikiwa kwa kuwa wao ni vyanzo vya mgogoro ya ardhi kwa kuwa wanatengeneza migooro. Ameiomba ofisi ya ardhi kanda ya kaskazini  ambayo makao yake yapo mjini Moshi mkoani Kilimanjaro kupeleka afisa ardhi mteule wa wilayani Karatu ili kuepuka kutegemea afisa ardhi mteule wa Jiji la Arusha. Viongozi wa Bakwata wakiongozwa na mwenyekiti wa bakwata wilaya  Said Rashid,amekiambia kikao hicho kuwa walipewa kiwanja hicho na halmashauri ya wilaya mwaka 2000 na ilipofika mwaka 2001 waliibuka watu watatu ambao wakiongozwa na Erro barani,walidai wao ni wamiliki wa asili wa eneo hilo na kufungua kesi mahakaman wakiishitaki halmashauri pamoja na Bakwata . Amesema mara baada ya kupewa kiwanja hicho namba 27,chenye ukubwa wa 50 kwa 60 sawa na robo tatu ya hekari walilipa gharama zote ambazo ni shilingi milioni 14.5 Amesema wakati wanataka kuanza kuliendeleza walalamikaji walienda mahakamani na kupewa kibali cha kutokuondoka mpaka watakapolipwa fidia na halmashauri jambo ambalo halijatekelezwa hadi leo. Alipoulizwa na kamishina mkuu wa Ardhi ,Mary Makondo,iwapo Bakwata wapo tayari kupewa eneo lingine kama fidia tofauti na hilo walilopewa awali na halmashauri ya wilaya ,Mwenyekiti huyo alikataa na kusema kuwa Bakwata haipo tayari kupokea eneo mbadala. Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Karatu,Waziri Mourice ,amekiambia kikao hicho kwamba  eneo hilo ni mali ya Bakwata  na ndio waliomilikishwa kihalali na halmashauri na si vinginevyo na hao wanaolalamika hawakubali kufidiwa eneo lingine ndani ya halmashauri ya wilaya ya Karatu. MWISHO.

Comments

Tanzania

TAARIFA MBAYA KWA WAVUTAJI WA SIGARA, TUMBAKU

HOTUBA YA WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO, MHE. UMMY A. MWALIMU (MB), KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2018/2019

MADAI YA WAFANYAKAZI YASABABISHA VIFAA VYA UJENZI VYA KAMPUNI YA  CEYTUN KUZUIWA UWANJA WA NDEGE TABORA.