PROFESA MBARAWA AHIMIZA KASI YA UJENZI UBUNGO INTERCHANGE.


PROFESA MBARAWA AHIMIZA KASI YA UJENZI UBUNGO INTERCHANGE. Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amemtaka Meneja wa Wakala wa Barabara (Tanroads) mkoa wa Dar es Salaam , Uongozi wa Manispaa ya Ubungo na Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka (BRT), kushirikiana ili kuondoa vikwazo vyote vinavyomkabili mkandarasi anayejenga barabara za juu katika makutano ya ubungo (interchange). Akizungumza mara baada ya kukagua kazi za ujenzi zinazoendelea katika mradi huo Profesa Mbarawa amezungumzia umuhimu wa wadau hao kushirikiana ili kuwezesha eneo la ujenzi kuwa safi na salama wakati wote na hivyo kuongeza kasi ya ujenzi. “Hakikisha mifumo ya umeme, maji, mawasiliano ya simu na gesi iliyopita katika eneo la mradi huo inaondolewa haraka na kwa usalama bila kuathiri huduma kwa wananchi”, amesema Profesa Mbarawa. Profesa Mbarawa amekagua maabara ya kuchunguza udongo, ujenzi wa nguzo za barabara za juu, mtambo wa kutengeneza zege na barabara zitakazotumika wakati ujenzi ukiendelea na kuzungumzia umuhimu wanafunzi wengi wa mafunzo kwa vitendo kupewa fursa katika miradi mikubwa ya ujenzi ili kuongeza wataalam wazalendo. Aidha Profesa Mbarawa ameutaka uongozi wa Manispaa ya Ubungo kuwaondoa wafanyabiashara ndogondogo (machinga), katika eneo hilo ili kupisha kazi za ujenzi. Naye Meneja wa Tanroads mkoa wa Dar es Salaam Eng. Julius Ndyamukama amemhakikishia Waziri Profesa Mbarawa kuwa vikwazo vyote katika eneo la mradi vitaondolewa ikiwemo majengo yaliyopo ndani ya eneo la mradi katika kipindi kifupi. Kiasi cha shilingi bilioni 177 zinatarajiwa kutumika katika ujenzi wa barabara za juu katika eneo la Ubungo zinazojengwa na mkandarasi China Civil Engineering Construction Corporation kwa miezi thelathini na kukamilika kwake kutapunguza msongamano wa magari katikati ya jiji la Dare s salaam. Imotolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Comments

Tanzania

TAARIFA MBAYA KWA WAVUTAJI WA SIGARA, TUMBAKU

HOTUBA YA WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO, MHE. UMMY A. MWALIMU (MB), KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2018/2019

MADAI YA WAFANYAKAZI YASABABISHA VIFAA VYA UJENZI VYA KAMPUNI YA  CEYTUN KUZUIWA UWANJA WA NDEGE TABORA.