SMZ YAONGEZA PENCHENI YA WASTAAFU


Na Mwajuma Juma, Zanzibar SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imefanya maraekebisho ya pencheni kwa wastaafu ambapo sasa wazee hao watapokea shilingi 90,000 kwa mwezi kutoka 40,000 kwa wastaafu wote wa Zanzibar ambao ni 12,182. Kiwango hicho kipya kimetangazwa jana na Waziri wa Fedha na Mipango wa SMZ Dkt. Khalid Salum Mohammed alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari huko ofisini kwake Vuga mjini hapa. Alisema kuwa kiwango hicho kimeongezeka kwa asilimia 125 ambacho kinakwenda sambamba kiwango cha asilimia 30 kinachokatwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF). Dkt. Khalid alisema kuwa hatua hiyo imefanywa kwa lengo la kutekeleza ahadi yake aliyoitoa wakati akisoma bajeti ya Serikali katika kikao cha bajeti kilichopita, ambapo kiwango hicho kipya kilikuwa kinaanza utekelezaji wake Julai ya mwaka huu. Alifahamisha kwamba marekebisho hayo yalitarajiwa kuanza mwanzoni mwa mwezi wa Julai lakini ilishindikana kutokana na changamoto ya kupata tarifa za wastaafu hao kutoka Utumishi. Hivyo alisema kuwa pamoja na kuchelewa huko lakini kiwango hicho kipya kitaanza utekelezaji wake Julai mwaka huu, na utaratibu wa kuzirejesha utafanyika katika malipo yanayofata. “Kabla ya marekebisho hayo wastaafu hao walikuwa wakilipwa shilingi 40,000 kila mwezi na sasa watapokea shilingi 90,000 kutokana na kuongeza shilingi 50,000, hii tumefanya kw alengo la kuwasaidia katika hali yao ya kimaisha kama ilivyo kwa wafanyakazi”, alisema. Alifahamisha kwamba kiwango hicho kipya kitawahusu wale wafanyakazi wastaafu wa kawaida na hakiwahusu wastaafu ambao wamestaafu wakiwa na nyadhifa mbali mbali makazini mwao, ambao marekebisho yao na wao yamo katika mchakato. Hata hivyo alisema kuwa kiwango hicho kipya kimefanywa kufatia Serikali kutangaza kima cha chini cha mshahara kwa wafanyakazi Serikalini kufikia 300,000 kutoka 150,000.

Comments

Tanzania

HOTUBA YA WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO, MHE. UMMY A. MWALIMU (MB), KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2018/2019

Hatua za Ugonjwa wa UKIMWI

MAITI YAOKOTWA IKIWA KWENYE MFUKO, MIKONO NA MIGUU YAFUNGWA KAMBA KWA NYUMA