TFS KUPANDA MITI KATIKA HEKTA  LAKI 182 KILA MWAKA ILI KUKABILIANA NA UHARIBIFU WA MISTU NCHINI.


Na  Tiganya Vincent RS-TABORA 21 AGOSTI 2017 Wakala wa Huduma za Mistu Tanzanaia (TFS) imepanga kupanga miti katika hekta 182,000 kwa mwaka ili kukabiliana na uharibifu wa mistu ulitokana na shughuli mbalimbali za binadamu katika mistu ya hapa nchini. Kauli hiyo imetolewa jana na Afisa Mistu na Mtalaalamu , Mshauri wa Usimamizi na Uhifadhi wa Mistu wa TFS Dkt. Ismail Aloo wakati akiongea kwenye kikao cha utekelezaji wa randama ya ushirikiano wa usimamizi wa rasilimali za mistu kanda ya magharibi. Alisema kuwa hali ya uharibifu wa mistu hapa nchini inatisha ambapo hekta 372,000 kila mwaka zinaharibiwa kutokana na kilimo cha kuhama hama , uchomaji mkaa, mifugo isiyozingatia ufugaji bora na uchanaji mbao usiozingatia taratibu na sheria. Dkt. Aloo aliongeza kuwa  ili kukabiliana na tatizo hilo juhudi zaidi zinahitajika katika upandaji miti kwa ajili ya kuziba pengo la uharibifu wa mistu ambao  umeifanya Tanzania kuwa  uhaba miti kwa ujazo wa mita wa miti milioni 19. Kwa upande wa Mtendaji Mkuu wa TFS Mtendaji Mkuu wa (TFS), Prof. Dos Santos Silayo alisema kuwa ni marufuku kwa viongozi wa vijiji kuwaagiza wananchi kufekya mistu katika maeneo wanayomiki kwa kisingizio cha uendelezaji wa sehemu zao. “Watendaji wa Vijiji katika baadhi ya maeneo wanawalazimisha watu wanaomiliki maeneo ambayo yana miti kuifyeka kwa kisingizio cha kuendeleza eneo lao…hii sio sahihi”alisema Profesa Silayo. Alisema kuwa viongozi hao lazima watambue kuwa mistu ya hapa nchini ina thamani ni lazima wahakikishe wanaitunza kwa kusimamia sera na sheria na sio wao kuwa chanzo cha uharibifu. Akifungua kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri aliwaagiza Wakuu wa Wilaya mkoani Tabora kushirikiana na Watendaji wa TFS katika kuhakikisha wanasimamia Sera na Sheria katika kuwaondoa watu wote waliovamia mistu ya hifadhi. Alisema kuwa suala la kusimamia mistu na kuifanya iwe endelevu haliwezi kuwa TFS pekee bali linahitaji nguvu za pamoja ikiwemo kutoka katika Halmashauri husika. Bw. Mwanri alisema kuwa uharibifu ukiendelea katika mistu haitalaumiwa TFS pekee bali hata viongozi wengine katika maeneo husika watabeba lawama hizo. “Kama tutashirikiana  fahamu kuwa hakuna jambo ambalo litatushinda katika kukabiliana na watu wanaoharibu mistu na kutishia maisha ya wananchi” alisisitiza Mkuu huyo wa Mkoa. Aidha Mkuu huyo wa Mkoa aliwaagiza Watendaji mbalimbali kuanza kuelimisha wananchi umuhimu wa matumizi ya majiko sanifu yanayotumia mkaa kidogo ili kupunguza mahitaji ya nishati hiyo ambayo nayo ni miongoni mwa matishio ya mistu.

Comments

Tanzania

TAARIFA MBAYA KWA WAVUTAJI WA SIGARA, TUMBAKU

HOTUBA YA WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO, MHE. UMMY A. MWALIMU (MB), KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2018/2019

MADAI YA WAFANYAKAZI YASABABISHA VIFAA VYA UJENZI VYA KAMPUNI YA  CEYTUN KUZUIWA UWANJA WA NDEGE TABORA.