WAKUU WA WILAYA WAAGIZWA KUKAMATA NA KUTAIFISHA TUMBAKU INAYOUZWA KINYEMELA


WAKUU wa wilaya mkoani Tabora wameagizwa kukamata na kutaifisha tumbaku na malori yatakayokutwa yamepakia tumbaku na kwenda kuuzwa kinyemela nje ya utaratibu uliowekwa na serikali. Agizo hilo limetolewa jana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassimu Majaliwa alipokuwa akizungumza na wananchi katika mikutano ya hadhara iliyofanyika wilayani Sikonge na Urambo. Alisema zao la tumbaku ni muhimu sana kwa uchumi wa wananchi wa mkoa wa Tabora na maeneo mengine hapa nchini lakini utaratibu mbaya na mazoea ya baadhi wakulima kuuza kiholela haukubaliki. Alisema kuanzia sasa kila mkulima atatakiwa kuuza tumbaku yake katika chama chake cha msingi (AMCOS) na si vinginevyo na ni marufuku wauzaji binafsi (IF) na Associations au mtu yeyote yule kuuza nje ya utaratibu huo. ‘Wakuu wa wilayani kamateni tumbaku yote itakayouzwa kiholela nje ya utaratibu huu na malori yote yatakayotumiwa kubeba tumbaku hiyo yakamateni mara moja’, aliagiza. Aliagiza Maafisa Kilimo na Maafisa Ushirika wa halmashauri zote kusimamia kwa ukaribu zaidi kilimo cha zao hilo na kusajiri vyama vyote vya wakulima wa tumbaku Ili kuhakikisha agizo linatekelezwa aliiagiza kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Sikonge kuwaita na kuwaonya wanunuzi maarufu wanane ambao wamekuwa na tabia ya kununua tumbaku ya wakulima kinyume na utaratibu. Alibainisha kuwa wamekaa meza moja na makampuni wanunuzi wa zao hilo na kuafikiana tumbaku yote ambayo haijauzwa inunuliwe. Katika mikutano hiyo Waziri Mkuu alipiga marufuku uuzwaji wa zao hilo kwa kutumia fedha za kigeni (dola) na kuagiza wanunuzi wote kutumia shilingi kwa kuwa wakulima wamekuwa wakiibiwa pasipo kuelewa. Aidha aliagiza Wakuu wa wilaya kushirikikana kwa karibu zaidi na Wenyeviti wa halmashauri, Madiwani, Wakurugenzi na Watendaji wote ili kuharakisha maendeleo ya halmashauri zao ikiwemo kuinua kilimo cha zao. xxxxxxx

Comments

Tanzania

TAARIFA MBAYA KWA WAVUTAJI WA SIGARA, TUMBAKU

HOTUBA YA WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO, MHE. UMMY A. MWALIMU (MB), KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2018/2019

MADAI YA WAFANYAKAZI YASABABISHA VIFAA VYA UJENZI VYA KAMPUNI YA  CEYTUN KUZUIWA UWANJA WA NDEGE TABORA.