Watatu mbaroni kwa kukutwa na silaha kigoma


WATU watatu wanashikiliwa na Jeshi la polisi Mkoa Kigoma kwa tuhuma za kumiliki silaha moja aina ya SMG yenye namba 56-12803036 ikiwa na magazini moja ikiwa na risasi 08 pamoja na  risasi 30 huko Katika Wilaya ya Kakonko. Akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake Kamanda wa  polisi mkoani Kigoma, DCP Fredinand Mtui alisema Agost 16 mwaka huu katika Kijiji cha  Mgera  tarafa ya Muyama Wilaya ya Buhigwe, askari wakiwa  katika kizuizi  wakiendelea na upekuzi wa magari ilikuja Pikipiki moja  ambayo namba yake haikufahamika  ikielekea eneo ambalo mnada wa Kijiji hicho ulikuwa ukiendelea  ilikuwa na watu wawili wakiwa na mfuko  moja. Alisema watuhumiwa baada ya kuwaona Askari  waligeuza  pikipiki na kuanza kirudi walikotoka  na kutupa mzigo waliokuwa wameubeba, askari walipo pekua mfuko huo walifanikiwa kukuta silaha moja ya SMG  ikiwa na magazini moja nia risasi nane waliyokuwa wakimiliki Kinyume na utaratibu. Kamanda Mtui alisema katika tukio lingine  huko katika kijiji Cha Kasanda Wilaya ya Kakonko askari wakiwa doria walimkamata  Nyamweru Yunus (28) mkazi katika kambi ya Wakimbizi mtendeli akiwa na risasi 30 za silaha aina ya SMG kitendo ambacho ni kinyume na sheria. "Upekuzi wa tukio hilo bado unaendelea Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kwa hatua za kisheria pindi upelelezi utakapo kamilika,jeshi la polisi linawasihi wananchi wote kuendelea kutoa taarifa za watu wanao jihusisha na uhalifu ili hatua za kisheria ziweze  kuchukuliwa dhidi yao", alisema Kamanda Mtui. Mwisho.

Comments

Tanzania

TAARIFA MBAYA KWA WAVUTAJI WA SIGARA, TUMBAKU

HOTUBA YA WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO, MHE. UMMY A. MWALIMU (MB), KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2018/2019

MADAI YA WAFANYAKAZI YASABABISHA VIFAA VYA UJENZI VYA KAMPUNI YA  CEYTUN KUZUIWA UWANJA WA NDEGE TABORA.