WAZIRI MKUU AMEWATAKA WATUMISHI WA UMMA NENDENI VIJIJINI MKAWATUMIKE WANANCHI


WAZIRI MKUU AMEWATAKA WATUMISHI WA UMMA NENDENI VIJIJINI MKAWATUMIKE WANANCHI Na Tiganya Vincent Tabora Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amewaagiza watumishi wote wa umma kuondoka maofisa na kwenda vijijini kwa ajili ya kusikiliza kero mbalimbali za wananchi ambazo yanasababisha wasiendelee. Mhe. Majaliwa alitoa kauli hiyo jana wakati akiongea na watumishi wa Wilaya ya Uyi mkoani Tabora. Alisema kuwa wakisha kuwasiliza wananchi warudi Ofisi kwa ajili ya kujipanga namna ya kutatua kero na matatizo ya wananchi ambayo yanakwamisha juhudi zao ya kujiletea maendeleo. Waziri Mkuu alisema Serikali ya Awamu ya Tano ipo kwa ajili ya kuwatumikia wananchi wote na hivyo imetoa dhamana kwa watumishi wa umma wafanye kazi karibuni kwa kwenda vijijini ili kuwatumikia Watanzania wote. Aidha alionya kuwa Serikali hii haitawavumilia watumishi wa umma wenye tabia za urasimu katika kuwatumikia na kutatua kero mbalimbali za watanzania. "Serikali haitamvumilia mtumishi yoyote wa umma ambayo mwananchi anakwenda kwake kwa mara ya kwanza kueleza shida yake kisha anamwambia mwananchi arudi kesho na anaporudi kesho , anambia tena arudi kesho .....mwisho mwananchi anaanza kukata tamaa ya kusaidiwa tatizo lake" alisisitiza Waziri Mkuu. Alisema kuwa mwanachi anapofika katika Ofisi za Umma kwa ajili ya kutatuliwa tatizo lake asaidiwe haraka bila kuzungushwa zungushwa ili aone Serikali yake ipo kwa ajili ya kumsaidia. Mwisho

Comments

Tanzania

TAARIFA MBAYA KWA WAVUTAJI WA SIGARA, TUMBAKU

HOTUBA YA WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO, MHE. UMMY A. MWALIMU (MB), KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2018/2019

MADAI YA WAFANYAKAZI YASABABISHA VIFAA VYA UJENZI VYA KAMPUNI YA  CEYTUN KUZUIWA UWANJA WA NDEGE TABORA.