Posts

Showing posts from September, 2017

MBOLEA KUTOKA NJE YA NCHINI IWE CHACHU YA KILIMO CHENYE TIJA

Jovina Bujulu-MAELEZO Hivi karibuni, Serikali kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Ubora wa Mbolea (TFRA) imeingiza nchini mbolea yenye uzito wa tani 55,000 kwa mfumo mpya wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja bila kuwepo malipo ya ziada bandarini. Mfumo huo utasaidia kupunguza bei na kuhamasisha matumizi ya mbolea kwa wakulima wengi nchini. Uingizwaji wa mbolea hiyo ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba alipokuwa akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya wizara hiyo kwa mwaka 2017/18, mjini Dodoma. DKt. Tizeba alisema kuwa kuanzia msimu wa 2017/18 Serikali itaanza kuagiza mbolea kwa mfumo wa pamoja kwa kuanza kuagiza aina mbili za mbolea ambazo ni mbolea ya kupandia (DAP) na ya kukuzia (UREA), kwa kuwa ndizo zinatumika sana nchini. Alitaja sababu za kutumia mfumo huo kuwa ni pamoja na kuongeza matumizi ya mbolea nchini kwa kuhakikisha kuwa wadau wote wanapata uhakika wa upatikanaji wa mbolea kwa bei ya ush…

'MASHETANI' YAVAMIA MSIKITI, YAJERUHI MLINZI NA KUPORA VITU

Image
Na Mwandishi wetu, Igunga. WATU sita wanaosadikika kuwa ni majambazi (MASHETANI) wamevamia msikiti mkuu wa ijumaa uliyoko kata ya Igunga mjini wilayani hapa mkoani Tabora kisha kumjeruhi mlinzi na kupora baadhi ya vitu ikiwemo vitabu vya dini ya kiislamu. Mlinzi aliyejeruhiwa ni Juma Mussa (55) mkazi wa mtaa wa Nkokoto kata ya Igunga wilayani hapa ambaye amelazwa katika hospitali ya wilaya ya Igunga wodi No. 8 na hali yake bado ni mbaya. Akizungumza kwa shida akiwa wodini mlinzi huyo alisema tukio hilo limetokea September 25 mwezi huu majira ya saa 8 usiku ambapo watu hao walifika msikitini hapo kisha kurusha jiwe kwenye eneo alilokuwa amekaa. Alisema baada ya kuona jiwe hilo ndipo aliamua kusimama ambapo muda mfupi jambazi moja liliruka uzio wa msikiti kisha likaingia na kuanza kumshambulia kwa mapanga kichwani. Alibainisha kuwa wakati akishambuliwa yeye aliona majambazi wengine wakifungua milango ya msikiti huo huku mmoja wa majambazi hao akimwambia mwenzake kuwa wewe m…

MARUFUKU SHULE MKOANI SINGIDA KUNUNUA CHAKI NJE YA MKOA

Image
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi Na Mwandishi wetu, Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi amepiga marufuku Shule zote Mkoani Singida kuagiza chaki nje ya Mkoa kwakuwa kuna viwanda vinavyozalisha chaki bora mkoani hapa. Dkt Nchimbi ametoa katazo hilo mara baara ya kufanya ziara katika viwanda viwili vinavyozalisha chaki katika halmashauri ya Itigi na kushuhudia chaki yenye ubora ikiwa imezalishwa kwa wingi na ikiwa haijapata soko. “Hawa wenye viwanda wamejitahidi kuzalisha chaki bora haina vumbi na inauzwa kwa bei sahihi lakini shule zetu badala ya kuja kununua hapa ambapo ni karibu wanaagiza Dar es salaam na mikoa mingine”, amesema na kuongeza kuwa, “Yani mnasubiri chaki hii hii iende Dar es Salaam halafu mnainunulia kutoka huko, hii haikubaliki, kuanzia leo shule zote zinunue chaki hapa hapa ili tupunguze gharama pamoja na kuinua viwanda vyetu”. Dkt Nchimbi ameongeza kuwa Mikoa ya Jirani itakayonunua chaki katika Viwanda vya Singida, vitasafirishiwa chaki…

Alitoka kijijini kuja Dar kufanya kazi, akaishia kubakwa akapachikwa mimba na Ukimwi

Image
MSICHANA mmoja mwenye mkazi wa Kata ya Pangani, Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani ameambukizwa virusi vya Ukimwi baada ya kubakwa akiwa amelala chumbani kwake na jirani. Taarifa zinasema msichana huyo alikuwa katika eneo hilo kama mfanyakazi wa ndani, na wakati anabakwa mabosi wake walikuwa nje ya nyumba aliyokuwa anaishi; kwamba walikuwa na makazi maeneo mengine, hivyo binti aliachwa katika nyumba hiyo akiwa peke yake. Ndipo jirani, alianzisha tabia ya kumbaka. Msichana huyo anasema alibakwa mara mbili; siku ya kwanza mbakaji alivunja mlango na kumuingilia kwa nguvu huku akimtishia kumuua kama angesema kwa watu au kupiga kelele. Siku nyingine mbakaji alirudia tena kumbaka. Kwa mujibu wa mbakwaji ni kwamba ubakaji huo ulikuwa unafanyika wakati huo mke wa mbakaji alipokuwa safarini. Mke wa mbakaji na mbakwaji ni marafiki wazuri. Mke aliporudi siku moja wakiwa pamoja, mbakwaji alianza kutokwa machozi, ndipo mke wa mbakaji alipomuuliza kulikoni rafiki yangu mbona unalia. Hapo ndipo s…

Uchawi wasababisha watu sita kuhukumiwa adhabu ya kunyongwa hadi kufa

> > NDUGU sita wa familia moja wamehukumiwa kifo kwa kunyongwa baada ya kuthibitika Kuwa walimuua ndugu yao wakimtuhumu Kuwa ni mchawi. > > Ndugu hao walihukumiwa Jana na mahakama kuu ya kanda ya Sumbawanga baada yakuridhika na upande wamashtaka Kuwa walitendakosa hilo. > > Jaji Wa Mahakama hiyo, Dk Adam Mambi alisoma hukumu hiyo ambapo alisema kuwa pasipo kuacha shaka watuhumiwa walifanya mauaji ya ndugu yao huyo. > > Waliokutwa na hatia katika shauri hilo ni Ferdinand Kamande, Peter Mpandisharo, Edes Kamande, Stephen Sikanda, Henrick Nguvumali Anatory Kamande huku watuhumiwa Alistid Kamande na Will broad Kamande wakiachiwa huru kwa kutokutwa na hatia Katika shtaka hilo. > > Katika shauri hilo upande wa mashitaka uliongozwa na mawakili wa serikali ambao ni Scolastica Lugongo na Adolf Lema huku upande wa utetezi ukiwakilishwa na wakili Mathias Budodi, ambapo ilidaiwa kuwa washitakiwa walifanya mauaji hayo Septemba 27, mwaka 2014. > > Awali Iliel…

BOHARI YA TPC YATEKETEA KWA MOTO

BOHARI ya kuhifadhia vifaa mbalimbali katika Kiwanda cha Sukari cha TPC Kilichopo Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro,imeteketea kwa moto na kusababisha hasara kubbwa kwa kiwanda hicho. Bohari hiyo ya kutunzia vipuri vya mashine na vipuri vya vifaa mbalimbali vinavyohusiana na vifaa vya mashambani,iliteketea Septemba 26 majira ya saa Nane usiku. Akizungumza kwa njia ya simu, afisa utawala Mkuu wa kiwanda cha TPC, Jafary Ally,alithibitisha kutekeketea kwa vipuri hiyo vilivyokuwa vimehifadhiwa katika boharai hiyo,na kueleza kuwa waliweza kuudhiiti moto huo ndani ya saa mbili. Kwa mujibu wa ally, moto huo umetekeketeza sehemu kubwa ya bohari kuu ya kiwanda hicho na kwa sasa jitihada za kufanya tathimini ya hasara iliyopatikana zinaendelea kufanyika. “Ni kweli tumepata ajali ya moto hapa kiwandani na stoo yetu kuu imeteketea kwa moto, na kimsingi ni kwamba tukio hili halijawahi kutokea kwa zaidi ya miaka 26, ni tukio liliosababisha hasara kubwa sana ambayo haijawahi kutokea”alisema.…

Ardhi, World Bank, and DFID collaborate to train next generation of disaster risk managers

Image
DAR ES SALAAM, September 26, 2017 – A newly scaled up 2nd phase of Ramani Huria, the mapping initiative by the World Bank, DfID, and several implementation partners, will engage 300 Urban Planning and Geomatics students from Ardhi University and equip them with skills to create sophisticated and highly accurate maps of localities around Dar es Salaam. The Ramani Huria scale up which was launched today in Dar es Salaam will employ community knowledge, elevation measurements, and drainage modelling to better understand where flooding has happened in the past, where it may happen in the future, and what mitigation actions will be required. Students will receive training and heavily transferable skills in GIS as they work to collect data on Dar es Salaam’s drainage, health care services, toilets, water sources, and various elements of urban infrastructure within 40 city wards. A Memorandum of Understanding signed between the World Bank and Ardhi University at the launch ceremony lay…

Dkt.Bendera kuzindua masafa ya Sunrise radio

Na Mwandishi wetu MKUU wa Mkoa wa Manyara,Joel Benbera anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa masafa mapya ya Redio Sunrise Fm,uzinduzi utaoenda sambamba na bonanza kubwa kabisa la michezo,katika uwanja wa Kwaraa,Babati,Mkoani Manyara. Akizungumza na vyombo vya Habari jana,Meneja wa Kituo cha Redio Sunrise,Ezra Agola,amesema kuwa uzinduzi huo utafanyika tarehe 29 katika uwanja huo na kwamba kituo hicho kitarusha matangazo yake Mkoa wa Manyara na maeneo ya jirani kupitia masafa ya 100.3 Fm. Meneja huyo amesema kuwa maandalizi kwa ajili ya uzinduzi yamekamilika na kuwataka wasikilizaji wote na wananchi kwa ujumla kujitokeza kwa wingi katika uwanja huo ambapo amesema kuwa kwa upande wa bonanza kutakuwa na michezo ya soka,riadha na mpira wa pete. “Katika tukio hilo timu nzima kuanzia menejimenti na wafanyakazi wote wa Sunrise redio watakuwepo,wasikilizaji,wapenzi,wanasalamu na wadau wote wa redio hii na matangazo yatarushwa moja kwa moja kutoka uwanjani hapo”alisema Agola …

Fuatilia Gari Lako Kwa Shs 1000/=

Image
Do you wish to Track your Trucks & Cars from your Phones? Ndiyo ! Kufuatilia gari lako lilipo kwa kiwango cha chini kuanzia Tsh 1000 tu kwa siku. Magari aina zote unaweza kufuatilia - Gari Ndogo, Lori na vile vile Boda Boda. 1. Je unataka kuokoa pesa kwenye magari ama boda boda? 2. Je unajua unaweza kufuatilia kuanzia gari moja mpaka magari 1000? 3. Je unataka kujua gari lako lilipo na wakati wowote? 4. Je unataka kuboresha huduma zako? 5. Je unataka kupunguza wizi au uharibifu wa magari? 6. Je unataka kujua tabia za Dereva wako? 7. Je unataka kupunguza ajali? 8. Je unataka kuwa na amani? Tuna ufumbuzi kutoka kwa Power Truck ya Power Computers Kwa kutumia simu za Android na Iphone unaweza kupata taarifa za mwenendendo wa gari lako kwa kubonyeza tu simu yako. Na pia unaweza kufuatilia gari lako lilipo Mtandaoni kwa kutumia kompyuta. ---------- Tupigie kwa ajili ya majaribio. Powertrack –Ni sehemu moja ya pekee ambapo utapata majibu yote kuhusiana na ufuatiliaji na udhibiti …

UN International Day of Peace at Mwembe Yanga Grounds in Temeke on 23rd of September, 2017.

Dar es Salaam September 21, 2017 The United Nations Information Centre (UNIC) in partnership with peace stakeholders in Tanzania including, The Jane Goodall’s-Roots& Shoots, Global Network of Religions for Children (GNRC),Global Peace Foundation, The Inter Religious Council for Peace in Tanzania, Tanzania Bora Initiative, Tanzania Scouts Association, Voluntary Service Overseas (VSO), Africa Centre for Peace and Conflict Research (ACPCR) and Youth of United Nations Association, are organizing the commemoration of the UN International Day of Peace at Mwembe Yanga Grounds in Temeke District on the 23rd of September, 2017. The International Day of Peace is commemorated each year on the 21st of September and the theme of the 2017 International Day of Peace is, Together for Peace: Respect, Safety and Dignity for All. The participants have invited the Inspector General of Police, Hon. Simon Sirro to be the Guest of Honor at the event which will focus on peace as an opportunity for yout…

DOKTA MPANGO AIHIMIZA WAINGEREZA KUKUZA ZAIDI BIASHARA NA UWEKEZAJI NCHINI

Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam Tanzania imetoa rai kwa Serikali ya Uingereza kubadili mfumo wa uhusiano wake kwa kujikita zaidi katika masuala ya biashara na uwekezaji badala ya kutoa misaada ya kawaida ili nchi iweze kukuza uchumi wake kwa haraka zaidi. Wito huo umetolewa Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango, alipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa wabunge kutoka mabunge ya uingereza (Baraza la Mamwinyi na Bunge la Wawakilishi). Dokta Mpango amesema kuwa kiwango cha mtaji ambacho Serikali ya Uingereza imewekeza nchini hadi sasa ni Paundi bilioni 2.5 lakini kwa upande wa biashara kati ya nchi hizo mbili, hali si nzuri. "Mwaka 2015 Tanzania iliuza nje bidhaa zenye thamani ya Dola za Marekani milioni 22.5 na kununua bidhaa kutoka Uingereza zenye thamani ya Dola milioni 150, kiwango ambacho ni kidogo sana na tunahitaji kufanya biashara zaidi" Alisisitiza Dkt. Mpango. Alielezea hatua mbalimbali ambazo Serikali inazichu…

TACAIDS: UKIMWI BADO NI CHANGAMOTO

Image
Kaimu Mkrugenzi Mkuu wa TACAIDS Bw.Jumanne Issango akieleza jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa mkutano kuhusu changamoto na mafanikio katika kupambana na ukimwi nchini uliofanyika katika ukumbi wa ofisi za TACAIDS leo Jijini Dar es Salaam. Na Fatma Salum – MAELEZO 21/09/2017 Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) imeendelea kuiasa jamii kuhusu kubadili tabia ili kuepuka maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwani ugonjwa huo bado ni janga kwenye nchi yetu. Hayo yamesemwa leo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa tume hiyo Bw.Jumanne Issango alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu mafanikio na changamoto za tume tangu ilipoanza kutekeleza majukumu yake. “UKIMWI bado ni changamoto katika maendeleo ya Taifa letu na umeendelea kuathiri kila sekta, kila imani, matajiri na masikini nchini kote hivyo ni wajibu wa kila mmoja kujitathmini mwenendo wake na kuacha tabia hatarishi ambazo zinachangia kuongeza maambukizi ikiwemo uasherati, ngono zembe, …

East and Southern Africa fertilizer and agribusiness leaders come to Maputo to discuss how to boost regional food security and prosperity

East and Southern Africa fertilizer and agribusiness leaders come to Maputo to discuss how to boost regional food security and prosperity The leaders of fertilizer production and trade from across the region will all be participating in discussions LONDON, United Kingdom, September 21, 2017/ -- In two weeks over 300 visitors from 28 different countries will join senior government figures and leading industry executives in Maputo, Mozambique. They will all gather to discuss the technical and commercial challenges facing the fertilizer and agribusiness industries in the region. The event is a three-day conference, including a gala reception hosted by OCP Africa, and is organized by CRU (www.CRUgroup.com) (a leading, independent, global fertilizers analysis, consultancy and events business) and The African Fertilizer Agribusiness Partnership (AFAP) (www.AFAP-Partnership.org). The conference opens with keynote addresses from the Government of Mozambique, a former commissioner of the Af…

Unataka maisha bora mwoga wa kujaribu, utafanikiwaje?

Na Dismas Lyassa HUWEZI kufanikiwa kama huthubutu kufanya mambo fulani. Kusoma sana au kidogo, kuwa na rafiki waliofanikiwa au wasiofanikiwa, kwenda nje ya nchi au la, au kuzaliwa familia maskini au tajiri, bado sio tiketi ya kukufanya uwe na maisha bora. Msingi wa kufanikiwa ni kuthubutu kufanya jambo fulani, kwa mfano kufungua mradi na mambo mengine kama haya. Kuna watu kwa mfano unaweza kuona anakata tamaa kwa sababu labda amezaliwa katika familia maskini, kitu ambacho sio sahihi. Msingi wa kuwa na maisha bora ni kufanya kazi kwa bidii na zaidi ni kuishi kwa malengo. Usiishi tu ili mradi siku zinakwenda mbele, ishi kwa malengo. Kwa chochote unachokifanya, kifanye baada ya kutafakari na kuangalia faida au hasara yake. Maisha yanatuhitaji kuwa waangalifu na wanadamu wanaotunguka, kwa sababu walio wengi furaha yao ni kuona unakuwa hauna mafanikio. Kuna wengine kwa mfano kabla ya kufanikiwa anakuwa ni rafiki, lakini ukishafanikiwa, anakuwa mtu mbaya. Kuna mwingine hata ukimwanga…

Africa: Dangote begs public to help monitor and report unscrupulous truck drivers, sets up hotline for reports

Dangote begs public to help monitor, report unscrupulous truck drivers, sets up hotline for reports LAGOS, Nigeria, September 19, 2017/ -- The Management of Dangote Industries Limited (www.Dangote.com) has launched a passionate appeal to members of the public to assist in monitoring both the recklessness and the illegal haulage of contraband goods by some of his truck drivers. The company has also set up hotlines for the public to call in and report such truck drivers, with a promise to appropriately compensate calls that lead to arrest of errant drivers. Noting that the trucks belonging to Dangote Cement are only allowed to carry cement, high grade gypsum and coal, those belonging to Dangote Sugar (NASCON) are authorized to carry only salt and Dan Q seasoning. Press release from the company also revealed that trucks belonging to Agro Sacks, the bags producing arm of Dangote Group, can only carry bags, belonging to Dangote flour Mills, Wheat, Flour and Danvita. “The Management …

JPM aenda Arusha

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 20 Septemba, 2017 ameondoka jijini Dar Es salaam kuelekea mkoani Arusha kwa ziara ya kikazi. Mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro KIA,Rais Dkt. Magufuli ataanza ziara yake Mkoani Manyara kwa kufungua barabara ya Kia - Mererani yenye urefu wa kilomita 26, na kuzungumza na wananchi wa mkoa huo. Tarehe 23 Septemba 2017, Rais Dkt. Magufuli atatunuku Kamisheni kwa Maafisa wanafunzi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha. Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar Es salaam , Rais Dkt. Magufuli ameagwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mhe. Paul Makonda. Jaffar Haniu Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU Dar Es Slaam. 20 Septemba 2017.

HATIMAYE MGOGORO KATI YA WALIOKUWA WAFANYAKAZI YA KAMPUNI YA CEYTUN NA WAMIKILI WAKE UMEMALIZIKA NA WAMELIPWA MADAI YAO.

Na Tiganya Vincent RS-TABORA 20 Septemba 2017 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amefanikiwa kumaliza mgogoro kati ya waliokuwa wafanyakazi 11 wa Kampuni ya Ujenzi ya Ceytun iliyokuwa ikipanua Uwanja wa Ndege wa Tabora na wamiliki wake juu ya kulipwa madai ya malipo ya muda wa ziada na mapunjo ya mishahara. Mgogoro huo ulimalizika jana mjini Tabora baada ya Wamiliki wa Kampuni hiyo kukubali na kulipa madeni ya wafanyakazi wake ambapo malipo yalifanyika mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora na Mkuu wa Wilaya ya Tabora. Hatua hiyo ilifikiwa baada ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora kuamuru kuwang’anywa Hati za kusafiria za viongozi wake wawili wa Kampuni hiyo na kuzuiwa kwa vifaa vyake vya ujenzi baada ya kuonekana kuwa anataka kuondoka bila kulipa malipo ya wafanyakazi hao. Akizungumza mara baada ya Kampuni hiyo kuwalipa waliokuwa wafanyakazi wake Mwanri alisema kuwa amelizika na kazi iliyofanyika na hivi sasa wanaweza kuchukua hati zao za kusafiria na wako huru kuondoa vifaa vyao vya uj…

WATU SABA WANASHIKIRIWA NA POLISI KWA TUKIO LA KUWATENDEA UNYAMA WANAWAKE WANNE

Na Tiganya Vincent RS –TABORA WATU saba wa kijiji cha Mwambondo wilayani Uyui wanashirikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kuwashambulia na kuwauunguza kwa moto wanawake waanne wakiwatuhumu kuwa wachawi na wanahusika na kifo cha mume wa mmoja wao. Kauli hiyo imetolewa jana mjini hapa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati wa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu taarifa alizozipata kutoka kwa Kamanda wa Polisi Mkoa huo Wilbroad Mtafungwa. Alisema kuwa chanzo cha vitendo hivyo vya kinyama zilianzia baada ya Mtu mmoja alikuwa akiitwa Mafumba Jirawisi kufariki kwa sababu ya maradhi lakini baadhi ya watu walianza kumtuhumu mke wa marehemu anayeitwa Manugwa Lutema kuhusika na kifo cha mume wake na kuamua kumpeleka porini na kuanza kumshambulia huku wakitaka awaeleze watu wanaoshirikiana naye kuwafanya vitendo vya kichawi. Mwanri alisema kuwa mama huyo baada ya kupiga sana na kuumia aliamua kutaja ovyo majina ya majirani zake na ndipo nao wakaunganishwa naye na kuen…

MLINZI WA AMANI KUTOKA TANZANIA AUAWA NCHINI CONGO

Statement attributable to the Spokesman for the Secretary-General on the Democratic Republic of the Congo NEW YORK, 18 September 2017- The Secretary-General condemns the killing of a Tanzanian peacekeeper serving with the United Nations Stabilization Mission in the Democratic Republic of the Congo (MONUSCO) on 17 September in Mamundioma, in North Kivu province, following a clash with suspected members of an armed group, the Allied Democratic Forces (ADF). Another peacekeeper was also injured during the incident. The Secretary-General offers his condolences to the friends and families of the deceased and to the Government of the United Republic of Tanzania. He wishes a speedy recovery to the injured and urges the authorities of the Democratic Republic of the Congo to swiftly investigate this incident and bring the perpetrators to justice. The Secretary-General calls on all armed groups in the Democratic Republic of the Congo to cease violence and to avoid a further deterioration…

RC AWATUPA MAHABUSU WATUMISHI 5 AWASIMAMISHA KAZI

RC AWATUPA MAHABUSU WATUMISHI 5 AWASIMAMISHA KAZI Na Allan Ntana, Igunga. Mkuu wa mkoa Tabora Agrrey Mwanri amewaweka mahabusu na kuwasimamisha kazi watumishi watano wa halmashauri ya wilaya ya Igunga kwa tuhuma ya kujipatia fedha Mil. 23,202,500 kwa njia ya udanganyifu mali ya halmashauri ya wilaya ya Igunga. Akizungumza jana na watumishi wa halmashauri ya wilaya Igunga katika ukumbi wa Maxwell alisema aliowasimamisha kazi ni pamoja na Kaimu Mganga mkuu wa wilaya ya Igunga Godfrey Mgongo(53), Mohamed Mtao afisa ugavi(49), Richard Byelembo aliyekuwa mhasibu wa idara ya afya kwa sasa ni mhasibu wa TATURA Igunga(36), Jones Lotho (57)Bohari wa Idara ya afya Igunga. Alisema kwa nyakati tofauti kati ya mwezi januari na machi 2017 watumishi hao wanne walikula njama na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu jumla ya Mil. 23,202,500 mali ya halmashauri ya wilaya ya Igunga. Aidha mtumishi wa tano aliyesimamishwa ni mganga mkuu wa zahanati ya kijiji cha Mwabakima kata …

UN General Assembly: Africa on social media

Dear All, In an effort to increase engagement by Africans in this year’s General Assembly, UN Department of Public Information- Africa Section requests you to find information contained in the attached promotional flyer. Our goal is to elicit public interest in General Assembly proceedings, particularly during the debate between 19 September and 22 September. A dedicated webpage (http://www.un.org/africarenewal/africaga2017) dubbed “Africa @ the UN General Assembly” has been created to provide visibility to Africa’s participation. For Africans, including the media, not directly participating in events in New York, the "Africa @ the UN General Assembly" is expected to be a one-stop source of information. Statements by African leaders, policy makers and social change activists and other pertinent reports will be uploaded on the webpage and on social media outlets, such as Twitter, Facebook and Flickr. Video clips and short interviews will also be publicised. Regards, S…

Tanzania Yachaguliwa Mwenyekiti Baraza la Uongozi la AMGC

Jonas kamaleki- MAELEZO Tanzania imechaguliwa kwa mara ya pili mfululizo kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Kituo cha Madini na Kijiosayansi cha Afrika (AMGC). Uchaguzi huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam katika Mkutano wa 37 wa Baraza hilo uliofunguliwa jana na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wajumbe wa Mkutano huo ambao ni mawaziri wa wanaohusika na sekta ya Madini wameipitisha Tanzania kwa kauli moja kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Baraza hilo kutokana na juhudi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais John Pombe Magufuli wa kudhibiti na kusimamia raslimali Madini pia mabadiliko yanayofanywa kituoni hapo. Akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la AMGC, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Prof. James Mdoe amesema Tanzania inathamini mchango wa Kituo hicho na kuongeza kuwa ndio maana Waziri Mkuu alifungua Mkutano wa Baraza. Prof. Mdoe amewakumbusha nchi wanachama…

TAARIFA KUTOKA TIBU BORA TANZANIA NA AFRIKA, SIMBA....

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Klabu ya Simba inawatangazia waandishi wote wa habari za michezo,kuwa kesho siku ya Jumatatu 18/9/2017 kutakuwa na mkutano . Mkutano huo utafanyika kwenye ukumbi mdogo wa klabu kuanzia majira ya saa 6 mchana,pamoja na mengine yatakayozungumzwa hiyo kesho,mkutano huu ni muhimu sana kwako/kwenu kuhudhuria kwani kuna mengi ya umuhimu ya kuyatolea ufafanuzi na kuyaweka wazi kwa umma wa mashabiki na wanachama wetu kupikia kwako/kwenu. Tunasisitiza kuwahi,kwani mkutano huo utaanza katika muda uliotajwa hapo juu na utazingatia muda. Mwisho Klabu inapenda kuwapa taarifa rasmi,kuwa kuanzia sasa kila siku ya Jumatatu tu tutakuwa na mkutano na nyinyi/wewe kuanzia majira ya saa 6 mchana kwenye ukumbi wa klabu,hivyo basi ni vyema mkaiongeza ratiba hii kwenye ratiba zenu za kazi za kila siku . Imetolewa na Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano Haji S. Manara. Simba Nguvu Moja..!!!

CHADEMA WAMZUIA NYALANDU KUMUONA LISSU, AISHIA KUPIGA PICHA NJE YA HOSPITALI

Image
Lazaro Nyalandu amezuiwa kumuona Tundulisu, katika hospital Nchini Kenya Matokeo yake nyalandu ameishia kupiga picha nje ya hospital hiyo na kusubiri usiku ufike Kama Doctors watamruhusu kwenda kumuona. Binafsi nampongeza nyalandu Kwa kuchukua jukumu la kumtembelea Tundu Lissu. Baadhi ya watu wanasema kwamba huu sio wakati wa kuweka vipingamizi vya kumuona kwa kisingizio cha usalama, kwani chumba alicholazwa Tundu Lissu kina ulinzi wa kutosha zikiwemo camera za CCTV ambazo watu huwangalia wagonjwa wakiwa sehemu maalum kama wana wasiwasi za usalama wao.

Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kukutana kesho

Image
KIKAO cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, kinatarajiwa kufanyika kesho Septemba 18 mwaka huu, chini ya Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein. Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar wa Idara ya Itikadi na Uenezi Mhe. Waride Bakari Jabu, imesema kikao hicho cha siku moja kitafanyika katika Ukumbi wa Afisi kuu ya CCM, Kisiwandui kuanzia saa 4:00 asubuhi. Pamoja na mambo mengine, kikao hicho kitapokea na kujadili kwa kina taarifa ya Hali ya Kisiasa ya Zanzibar pamoja na taarifa nyengine mbali mbali kutoka Idara na Vitengo vya Chama Cha Mapinduzi Zanzibar, vile vile kikao hicho kitapokea na kujadili majina ya wana CCM waliojitokeza kuomba kuteuliwa kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa CCM katika ngazi za Wilaya kwa kipindi cha 2017-2022, kwa upande wa Zanzibar na kutoa mapendekezo yake kwa Halmashauri Kuu ya Taifa. Kikao hicho kilitanguliwa na kikao cha Sekretarieti ya Kamati Maa…

Kazi ya kutoa huduma ni ngumu-Naibu spika

Na Mwandishi wetu, Zanzibar NAIBU Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mgeni Hassan Juma amesema kuwa kazi ya utoaji huduma kwa jamii ni nguvu na inahitaji uvumulivu na moyo wa huruma ili kufanikiwa. Alisema kuwa katika kazi hiyo unakutana na watu wenye tabia tofauti na kama huna moyo huwezi kudumu nayo au utajikuta ukiingia katika lawama kila siku kama ilivyo hivi sasa katika kada ya wauguzi na wakunga. Juma aliyasema hayo alipokuwa akifunguwa kongamano la siku moja la kujadili kushuka kwa maadili ya wakunga na wauguzi. Hata hivyo alisema kuwa changamoto kubwa iliyopo hivi sasa katika utoaji wa huduma hasa ni lugha kwa wagonjwa ambayo hutolewa na wauguzi na wakunga. Alisema lugha ni sehemu ya kutoa huduma kwa mgonjwa ambayo humfariji hata kabla ya kupatiwa matibabu. Aidha alisema kuwa kazi ya uuguzi na ukunga ni ya kujitolea na inahitaji kuwa na moyo ili kuweza kutoa huduma kwa jamii . Hivyo aliwataka wauguzi hao na wakunga ambao wanafanya kazi hiyo kuwa mabalozi wa kuwa…

7,578 wachaguliwa kujiunga ualimu Astashahada na Stashahada

Image
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako. WIZARA ya Elimu Sayansi na Teknolojia imetangaza Jumla ya waombaji 7,578 waliochaguliwa kujiunga na mafunzo ya ualimu katika ngazi Astashahada na Stashahada katika vyuo vya serikali vya ualimu kwa mwaka wa masomo 2017/18 huku nafasi nyingine zikibaki wazi. Kutokana na nafasi hizo kubaki wazi Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NECTA) linatoa fursa ya kuwasilisha maombi kwenye program za Astashahada na Stashahada katika fani mbalimbali nchini za ualimu. Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari ofisini kwake mjini hapa Katiku Mkuu wa Wizara hiyo Dr.Leonard Akwilapo alisema kuwa uchaguzi huo umezingatia vigezo vya jumla ambavyo ni ufaulu wa daraja la I hadi la III kwa Astashahada na Stashahada. Alisema kuwa waombaji wa Astashahada walifaulu masomo ya sayansi katika kidato cha nne walipewa kipaumbele, ikiwa ni daraji la I, alama 14 ambapo ufaulu wa chini ni daraja la III alama 25, na kw…

Waziri ajibu tuhuma kuhusu uhusiano wa Tanzania na Korea Kaskazini

Image
Pix 01: Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga (katikati) akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari wakati akitoa ufafanuzi juu ya tuhuma za Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu ushirikiano wa Tanzania na Korea ya Kaskazini mapema hii leo jijini Dar es Salaam. Pix 02: Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga (katikati) akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati akitoa ufafanuzi juu ya tuhuma za Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu ushirikiano wa Tanzania na Korea ya Kaskazini, kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Aziz Mlima na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha Wizara hiyo Bi. Mindi Kasiga. Pix 03: Mwandishi wa Habari toka kituo cha Televisheni cha Channel Ten, David Ramadhan akimuuliza swali Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga (aliye kaa katikati) wakati Waziri huyo akitoa ufafanuzi…

BRAZIL YAFUNGUA MILANGO YA BIASHARA NA TANZANIA; ILIFUNGWA KWA MIAKA MINGI KUTOKANA NA TANZANIA KUSHINDWA KULIPA DENI

Image
PICHANI NI Picha ya kwanza ni Kiongozi wa Korea kaskazini, Kim Jong Un -Picha zinazofuatia chini yake ni Balozi Dkt. Emmanuel J. Nchimbi akisaini Mkataba kwa niaba ya Serikali ya Jamnhuri ya Muungano wa Tanzania wa Msamahawa Deni la Tanzania kwa Serikali ya Brazil. Kwa upande wa Brazil mkataba huo ulisainiwa na Dkt. Sonia Nunes, Wakili wa Serikali ya Brazil. -Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akibadilishana mkabataba huo na Dkt. Sonia Nunes, Wakili wa Serikali ya Brazil mara baada ya kusaini mkataba wa msamaha wa deni. -Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiongoza ujumbe wa Tanzania katika mazungumzo na Serikali ya Brazil. -Balozi Dkt. Emmanuel J.Nchimbi pamoja na Mkuu wa Ujumbe wa Serikali ya Brazil Bw.Guilheme Laux (kulia kwa Balozi Nchimbi) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wapande zote mbili (Tanzania na Brazil) -Balozi Dkt. Nchimbi akiendelea na mazungumzo na ujumbe wa Serikali ya Brazil (Hawapo pichani) Serikali ya Brazil imesamehe Tanzania deni la jumla ya Dola za Mareka…

Prof. Elisante: Amani ni urithi unaopaswa kuendelezwa Afrika

Image
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akifungua mkutano wa kujadili utekelezaji wa Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika kati ya Tanzania na Afrika Kusini leo mjini Dodoma. Na Beatrice Lyimo- MAELEZO, DODOMA Watanzania wametakiwa kutunza, kulinda na kuimarisha amani na heshima iliyopo nchini kwani amani hiyo huifanya Tanzania iheshimike na Mataifa mengine. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel wakati akifungua mkutano wa kujadili utekelezaji wa Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika kati ya Tanzania na Afrika Kusini unaofanyika mjini Dodoma. Prof. Elisante amesema kuwa suala la kutunza na kulinda amani iliyopo huanzia kwa wananchi wenyewe, hivyo, ili Tanzania iendelee kuheshimika ni buni kutunza na kulinda heshima na utamaduni uliopo kwani amani na heshima, vikitoweka huchukua muda mrefu kuijenga au kuirejesha. “Tanzania imeendelea kuheshimika na kuim…

MADAI YA WAFANYAKAZI YASABABISHA VIFAA VYA UJENZI VYA KAMPUNI YA  CEYTUN KUZUIWA UWANJA WA NDEGE TABORA.

Na Tiganya Vincent RS-TABORA 14 AGOSTI 2017 KAMATI ya Ulinzi na Usalama mkoani Tabora imezuia vifaa vya ujenzi vya Kampuni ya Ujenzi ya Ceytun iliyokuwa ikipanua Uwanja wa Ndege na kuwang’anywa Hati za kusafiria za viongozi wake wawili hadi watakapomalizia malipo ya waliokuwa wafanyakazi wao. Waliokuwa wafanyakazi wa Kampuni hiyo ambao ni kumi wanadai milioni 20 ambazo malipo muda kazi ziada na mishahara. Uamuzi huo umetolewa jana mjini hapa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri alipokuwa akitoa maamuzi ya  wajumbe wake kwenye mkutano na viongozi wa Kampuni hiyo na wanaodai. Alisema kuwa wamefikia hatua hiyo baada ya Mhasibu wa Kampuni hiyo Bw. Mahmut Garik kukataa kutoa vielelezo vinavyoonyesha  jinsi alivyowalipa waliokuwa wafanyakazi wao ili kuona kama madai ya wafanyakazi hao ni halali au sio halali. Mwanri alisema kuwa zoezi la kushughulikia madai ya wafanyakazi hao ilikuwa ni sehemu ya utekelezaji maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungan…

SERIKALI KUENDELEZA MAHUSIANO NA WASHIRIKA WA MAENDELEO.

Na Beatrice Lyimo-MAELEZO, DODOMA Serikali imeahidi kuendelea kushirikiana na kujenga mahusiano mazuri na Washirika wa Maendeleo ili kuwezesha kufanikisha azma ya kushirikiana katika kuleta maendeleo nchini. Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati wa uzinduzi wa Awamu ya pili ya Mradi wa kulijengea uwezo Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo mjini Dodoma. “Kwa nia ya kuhakikisha miradi kama hii inayofadhiliwa na Washirika wa Maendeleo inaleta tija, Serikali ya Tanzania itaendelea kushirikiana na kujenga mahusiano mazuri kwa lengo la kufanikisha azma katika kuleta maendeleo,” alisema Majaliwa. Aidha Majaliwa ameongeza kuwa Serikali itaendelea kusimamia na kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa miradi kama hii ili kuhakikisha masharti na vigezo mbalimbali vilivyowekwa vinazingatiwa wakati wa utekelezaji wake. Mbali na hayo waziri Mkuu amesema kuwa, Serikali inatambua umuhimu wa kushirikiana na Bunge ikiwa ni pamoja na kuendelea kulijengea uwezo Bunge hilo ili l…

Profesa Safari asema Chadema hakina fedha, aomba msaada Ujerumani na EU kumtibu Lissu

Image
Na Mwandishi wetu CHADEMA inaendelea na harakati za kutafuta njia za kumtibia Mbunge wake, Tundu Lissu anayepata matibabu Kenya. Mwanasiasa huyo inadaiwa alipigwa risasi tumboni na miguuni; hali yake imekuwa nzuri na wakati fulani kubadilika na kuwa mbaya. Kulingana na taarifa ya Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Profesa Abdalah Safari ni kwamba matibabu yake yanagharimu kiasi cha Sh 10 milioni kwa siku. Gharama hizi kwa mujibu wa Profesa Safari ni kubwa, lakini chama kimeapa kitafanya inachoweza ili matibabu yafanyike. “Kwa sababu ya ukweli kwamba matibabu haya ni gharama kubwa, tumeziomba jumuiya za kimataifa ikiwamo Ujerumani na Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU) kutusaidia matibabu”. Chama, kwa mujibu wa Profesa kimeunda kamati maalumu ya kuratibu michango na moja ya sehemu walizowasilisha maombi ni kwa Serikali ya Ujerumani na Umoja wa Ulaya. “Siwezi kusema hadi sasa nini tumejibiwa, lakini kamati inaendelea kufuatilia, Wajerumani ni ndugu zetu maana chama cha CDU ni marafiki zetu n…

Wadau waitaka serikali kutekeleza Sheria ya Upatikanaji wa Taarifa/Stakeholders call on government to implement the Access to Information Act

Duniani kote, sheria za upatikanaji wa taarifa zimebadilisha uhusiano uliopo kati ya wananchi na serikali. Wananchi wanapoelewa serikari yao inafanya nini, huweza kuchagiza maendeleo na wao wenyewe kunufaika. Wananchi wakiwa na taarifa za kutosha huweza kuchangia ipasavyo jitihada mbali mbali za maendeleo zenye kuleta maboresho ya jamii. Wakati mwingine, wanaweza kusaidia kufichua vitendo vya rushwa na uovu katika jamii zao. Mara nyingi upatikanaji wa taarifa huiwezesha serikali kuhakikisha mipango yake inaendana na hali halisi ya jamii. Pia taarifa huwasaidia watafiti kuchunguza zaidi na kutoa ufumbuzi wa matatizo sugu yanayozikabili jamii.     Wananchi huweza kuuona umuhimu wao pale wanapoweza kufuatilia yale yanayoendelea katika jamii zao, na kuyachukulia hatua. Jamii bora ni ile inayoendesha shughuli zake kwa uwazi, ushirikishwaji na uwajibikaji; na yenye mifumo ya kuwapatia wananchi taarifa kwa uharaka. Jamii kama hiyo huwapa wananchi nafasi ya kushiriki kwenye masuala ya kij…