7,578 wachaguliwa kujiunga ualimu Astashahada na Stashahada


Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako. WIZARA ya Elimu Sayansi na Teknolojia imetangaza Jumla ya waombaji 7,578 waliochaguliwa kujiunga na mafunzo ya ualimu katika ngazi Astashahada na Stashahada katika vyuo vya serikali vya ualimu kwa mwaka wa masomo 2017/18 huku nafasi nyingine zikibaki wazi. Kutokana na nafasi hizo kubaki wazi Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NECTA) linatoa fursa ya kuwasilisha maombi kwenye program za Astashahada na Stashahada katika fani mbalimbali nchini za ualimu. Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari ofisini kwake mjini hapa Katiku Mkuu wa Wizara hiyo Dr.Leonard Akwilapo alisema kuwa uchaguzi huo umezingatia vigezo vya jumla ambavyo ni ufaulu wa daraja la I hadi la III kwa Astashahada na Stashahada. Alisema kuwa waombaji wa Astashahada walifaulu masomo ya sayansi katika kidato cha nne walipewa kipaumbele, ikiwa ni daraji la I, alama 14 ambapo ufaulu wa chini ni daraja la III alama 25, na kwa Stashahada ni daraja la I alama 6 huku ufaulu wa chini ukiwa ni daraja la III alama 17 “Jumla ya waombaji 15,091 walikamilisha maombi yao,waombaji 12,152 sawa na asilimia 80.5 walikuwa na sifa stahiki za kujiunga na program za ualimu waliomba lakini jumla ya waombaji 2,939 sawa na asilimia 19.5 hawakuwa na sifa zinazotakiwa kujiunga na mafunzo hayo ya ualimu. “Ikumbukwe kuwa nafasi za mafunzo ya ualimu katika vyuo 30 vya ualimu vya serikali zilizotangazwa zilikuwa 9,106 ambapo kati ya hizo 5,375 kwa program ya Astashahada ya elimu ya ualimu, na 3,731 ni za Stashahada mbalimbali za elimu ya ualimu”alisema Dr. Akwilapo. Aidha alisema kuwa vyuo hivyo vinatarajiwa kufunguliwa sept 25 mwaka huu. Akizungumzia nafasi zilizobaki wazi Dr. Akwilapo alisema katika zoezi hilo jumla ya nafasi 1,528 zilibaki wazi katika vyuo vya ualimu vya serikali bila kijanzwa, na kuwa hiyo ni kutokana na jinsi ambavyo waaombaji walifanya uchaguzi wa vyuo. Alisema kuwa kutokana na nafasi hizo kubaki wazi NACTE inatoa fursa kwa waombaji ambao hawakufanikiwa kupangwa kwenye vyou na wale ambao walikuwa bado hawajaomba kutuma maombi ya kuanzia Sept 18 hadi Oct 1 mwaka huu. Dr. Akwilapo alitumia nafasi hiyo kutoa wito kwa wahitimu wa kidato cha nne na cha sita walio na sifa za kujiunga na mafunzo hayo kufanya uchaguzi sahihi kwa kuzingatia ufauli wao. Mwisho

Comments

Tanzania

HOTUBA YA WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO, MHE. UMMY A. MWALIMU (MB), KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2018/2019

Hatua za Ugonjwa wa UKIMWI

MAITI YAOKOTWA IKIWA KWENYE MFUKO, MIKONO NA MIGUU YAFUNGWA KAMBA KWA NYUMA