Alitoka kijijini kuja Dar kufanya kazi, akaishia kubakwa akapachikwa mimba na Ukimwi


MSICHANA mmoja mwenye mkazi wa Kata ya Pangani, Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani ameambukizwa virusi vya Ukimwi baada ya kubakwa akiwa amelala chumbani kwake na jirani. Taarifa zinasema msichana huyo alikuwa katika eneo hilo kama mfanyakazi wa ndani, na wakati anabakwa mabosi wake walikuwa nje ya nyumba aliyokuwa anaishi; kwamba walikuwa na makazi maeneo mengine, hivyo binti aliachwa katika nyumba hiyo akiwa peke yake. Ndipo jirani, alianzisha tabia ya kumbaka. Msichana huyo anasema alibakwa mara mbili; siku ya kwanza mbakaji alivunja mlango na kumuingilia kwa nguvu huku akimtishia kumuua kama angesema kwa watu au kupiga kelele. Siku nyingine mbakaji alirudia tena kumbaka. Kwa mujibu wa mbakwaji ni kwamba ubakaji huo ulikuwa unafanyika wakati huo mke wa mbakaji alipokuwa safarini. Mke wa mbakaji na mbakwaji ni marafiki wazuri. Mke aliporudi siku moja wakiwa pamoja, mbakwaji alianza kutokwa machozi, ndipo mke wa mbakaji alipomuuliza kulikoni rafiki yangu mbona unalia. Hapo ndipo siri ilipoanza kufumuka. Binti alisema kwamba nalia kwa sababu mumeo amekuwa akinibaka wakati uko safarini. Kwamba, hiyo la kubaka limesababisha sasa nina mimba. Jambo hili lilileta kasheshe kubwa nyumbani, mke kumsaka mumewe ili ampachike maneno yanayomstahili kwa alichofanya. Vurugu ilikuwa kubwa baada ya wawili hao kuonana. Mume inasemekana alikiri kuchepuka njia kuu, na akatokomea nyumbani baada ya kuona hakuna maelewano. Akawa anarudi na kutoka. Baadaye suala hilo liliripotiwa Serikali ya Mtaa wa Mkombozi, Kata ya Pangani, ambao nao walilipeleka Polisi Kibaha ambako sasa wanamshikilia mtuhumiwa wa ubakaji. Baada ya vipimo zaidi ilibainika kwamba binti licha ya kubakwa na kupewa uja uzito, lakini pia ameambukizwa virusi vya Ukimwi. Haijulikani kama virusi hivyo vimetoka kwa mbakaji au mbakwaji alipita njia nyingine kabla ya kubakwa? Huenda uchunguzi wa polisi ukawa na majibu zaidi, kwani sasa tayari yuko mikononi wa polisi.

Comments

Tanzania

HOTUBA YA WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO, MHE. UMMY A. MWALIMU (MB), KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2018/2019

Hatua za Ugonjwa wa UKIMWI

MAITI YAOKOTWA IKIWA KWENYE MFUKO, MIKONO NA MIGUU YAFUNGWA KAMBA KWA NYUMA