BOHARI YA TPC YATEKETEA KWA MOTO


BOHARI ya kuhifadhia vifaa mbalimbali katika Kiwanda cha Sukari cha TPC Kilichopo Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro,imeteketea kwa moto na kusababisha hasara kubbwa kwa kiwanda hicho. Bohari hiyo ya kutunzia vipuri vya mashine na vipuri vya vifaa mbalimbali vinavyohusiana na vifaa vya mashambani,iliteketea Septemba 26 majira ya saa Nane usiku. Akizungumza kwa njia ya simu, afisa utawala Mkuu wa kiwanda cha TPC, Jafary Ally,alithibitisha kutekeketea kwa vipuri hiyo vilivyokuwa vimehifadhiwa katika boharai hiyo,na kueleza kuwa waliweza kuudhiiti moto huo ndani ya saa mbili. Kwa mujibu wa ally, moto huo umetekeketeza sehemu kubwa ya bohari kuu ya kiwanda hicho na kwa sasa jitihada za kufanya tathimini ya hasara iliyopatikana zinaendelea kufanyika. “Ni kweli tumepata ajali ya moto hapa kiwandani na stoo yetu kuu imeteketea kwa moto, na kimsingi ni kwamba tukio hili halijawahi kutokea kwa zaidi ya miaka 26, ni tukio liliosababisha hasara kubwa sana ambayo haijawahi kutokea”alisema. Aidha alisema kamati ya maafa ya kiwa hicho ipo katika jitihada za kukaa na kutathimini hasara ilitopatikana kutokana na ajali hiyo huku kiwanda hicho kikiendelea na uzalishaji wa sukari kama kawaidia. “Tunaendelea na uzalishaji kama kamawaida na tutahakikisha hatuta simamisha uzalishaji kwani kwa sasa jitihada iliyopo ni kuwasliana na bima ili kuona ni kwa namna gani tunapata vipuri kwa haraka zaidi”alisema Ally alipoulizwa kama tukio hilo linaweza kuhusishwa na hujuma, alisema haliwezi kuhusishwa na hujuma kutokana na kwamba mazingira iliyopo Stoo iliyoungua, yana ulinzi mkali ikiwemo wa Mbwa, na kwamba moto ulipoanzia ni ndani kwenye mitambo. Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro, Hamis Issah,alisema moto huo ulizuka majira ya saa 8:00 usiku na kwamba mpaka sasa thamani ya vitu vilivyoungua kutokana na moto huo bado haijajulikana. Kamanda Issah aliongeza kuwa uchunguzi unaendelea kufanywa ili kuweza kubaini chanzo cha moto huo ambao umesababisha hasara kwa kiwanda cha Sukari cha TPC. Mwisho

Comments

Tanzania

HOTUBA YA WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO, MHE. UMMY A. MWALIMU (MB), KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2018/2019

Hatua za Ugonjwa wa UKIMWI

MAITI YAOKOTWA IKIWA KWENYE MFUKO, MIKONO NA MIGUU YAFUNGWA KAMBA KWA NYUMA