Dkt.Bendera kuzindua masafa ya Sunrise radio


Na Mwandishi wetu MKUU wa Mkoa wa Manyara,Joel Benbera anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa masafa mapya ya Redio Sunrise Fm,uzinduzi utaoenda sambamba na bonanza kubwa kabisa la michezo,katika uwanja wa Kwaraa,Babati,Mkoani Manyara. Akizungumza na vyombo vya Habari jana,Meneja wa Kituo cha Redio Sunrise,Ezra Agola,amesema kuwa uzinduzi huo utafanyika tarehe 29 katika uwanja huo na kwamba kituo hicho kitarusha matangazo yake Mkoa wa Manyara na maeneo ya jirani kupitia masafa ya 100.3 Fm. Meneja huyo amesema kuwa maandalizi kwa ajili ya uzinduzi yamekamilika na kuwataka wasikilizaji wote na wananchi kwa ujumla kujitokeza kwa wingi katika uwanja huo ambapo amesema kuwa kwa upande wa bonanza kutakuwa na michezo ya soka,riadha na mpira wa pete. “Katika tukio hilo timu nzima kuanzia menejimenti na wafanyakazi wote wa Sunrise redio watakuwepo,wasikilizaji,wapenzi,wanasalamu na wadau wote wa redio hii na matangazo yatarushwa moja kwa moja kutoka uwanjani hapo”alisema Agola Amezitaja zilizothibitisha kushiriki kuwa ni Sunrise wenyewe,Parishi ya Galapo,Magugu Rangers,Vijana Stars na Usalama Babati na kuongeza kuwa timu nyingine zinaendelea kujitokeza ili kushiriki bonanza hilo. Meneja huyo aliongeza kuwa baada yakuzindua masafa hayo katika Mkoa wa Manyara,wataelekea Singida,Tabora,Mwanza ,Tabora na Geita lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa kitua hicho kinasikika nchi nzima. Alisema kuwa katika tukio hilo wasikilizaji wa redio hiyo watapata zawadi mbalimbali,na kwa upande wa bonanza washindi watapata zawadi mbalimbali ikiwemo mipira,jezi,nishani,fedha na kombe kwa washindi wa kwanza Mwishooooooooooo

Comments

Tanzania

TAARIFA MBAYA KWA WAVUTAJI WA SIGARA, TUMBAKU

HOTUBA YA WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO, MHE. UMMY A. MWALIMU (MB), KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2018/2019

MADAI YA WAFANYAKAZI YASABABISHA VIFAA VYA UJENZI VYA KAMPUNI YA  CEYTUN KUZUIWA UWANJA WA NDEGE TABORA.