Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kukutana kesho


KIKAO cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, kinatarajiwa kufanyika kesho Septemba 18 mwaka huu, chini ya Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein.
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar wa Idara ya Itikadi na Uenezi Mhe. Waride Bakari Jabu, imesema kikao hicho cha siku moja kitafanyika katika Ukumbi wa Afisi kuu ya CCM, Kisiwandui kuanzia saa 4:00 asubuhi. Pamoja na mambo mengine, kikao hicho kitapokea na kujadili kwa kina taarifa ya Hali ya Kisiasa ya Zanzibar pamoja na taarifa nyengine mbali mbali kutoka Idara na Vitengo vya Chama Cha Mapinduzi Zanzibar, vile vile kikao hicho kitapokea na kujadili majina ya wana CCM waliojitokeza kuomba kuteuliwa kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa CCM katika ngazi za Wilaya kwa kipindi cha 2017-2022, kwa upande wa Zanzibar na kutoa mapendekezo yake kwa Halmashauri Kuu ya Taifa. Kikao hicho kilitanguliwa na kikao cha Sekretarieti ya Kamati Maalum ya NEC - Zanzibar kilichofanyika Septemba 16, mwaka huu, chini ya Mwenyekiti wake Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dk.Abdulla Juma Saadalla “Mabodi”, kwa ajili ya kuandaa Ajenda za kikao hicho.

Comments

Tanzania

TAARIFA MBAYA KWA WAVUTAJI WA SIGARA, TUMBAKU

HOTUBA YA WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO, MHE. UMMY A. MWALIMU (MB), KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2018/2019

MADAI YA WAFANYAKAZI YASABABISHA VIFAA VYA UJENZI VYA KAMPUNI YA  CEYTUN KUZUIWA UWANJA WA NDEGE TABORA.