MARADHI YA SUKARI ZBAR TISHIO KWA WATOTO


Na Mwajuma Juma, Zanzibar DAKTARI Bingwa wa maradhi ya Kisukari Dkt. Faizar Kassim amesema kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la maradhi ya kisukari hasa kwa watoto waliochini ya umri wa miezi mitatu.   Alisema kuwa hali imekuwa ikitisha sana kutokana na idadi kuwa kubwa ambapo kila mwezi hujitokeza wagonjwa wapya wa kitoto kati ya 10 hadi 12.   Alifahamisha kwamba ongezeko hilo ni kubwa kulingana na miaka ya nyuma ambapo hadi 2007 jumla ya watoto wote walio na matatizo hayo walikuwa ni 33.   “Watoto sasa ndio tishio la ugonjwa huu, kwani mwaka 2007 ambapo ndio program ilianzishwa kwa ajili ya watoto walikuwa 33 na kuongezeka watoto 10 kwa mwaka na mwaka 2015 ongezeko la watoto kwa mwezi lilipanda hadi kufikia watoto sita kwa mwezi,  alisema Dkt. Faizar.   Hata hivyo alisema kuwa ongezeko la watoto kwa mwezi ilipanda na kupata watoto sita kwa mwezi katika mwaka 2016 lakini kwa mwaka huu limeongezeka zaidi hadi kufikia watoto 12.   Aidha alisema kuwa pamoja na ongezeko hilo lakini bado hawajajua nini tatizo lakini wanavyohisi tatizo kubwa kukosa lishe bora tokea wakiwa tumboni mpaka katika makuzi yao.   Hata hivyo alisema kuwa takwimu hizo ni kwa ajili ya kituo cha maradhi hayo Unguja tu lakini kwa Pemba watoto wenye matatizo hayo mpaka sasa ni 30, ingawa wengi wa watoto ambao wanpimwa wengine hutokea kisiwani humo.   Aidha alisema kuwa ili kujikinga na maradhi hayo hakuna budi kwa watu kufanya mazoezi lakini hakuna njia nyengine ya kujikinga nayo badala ya hiyo .   Akizungumzia kuhusu kuanzisha huduma ya kumkinga mtoto akiwa tumboni kama ilivyo kwa huduma za Ukimwi alisema kuwa hakliwezekani kwa sababu hayo sio maradhi ya kuambukiza.   “Kusema kweli inasikitisha sana kwani watoto hao ambao wanagundulika wengi wao hupoteza maisha kutokana na kutokuwa na kukosa huduma hasa pale wazazi baba na mama wakiwa hawaelewani”, alisema.

Comments

Tanzania

TAARIFA MBAYA KWA WAVUTAJI WA SIGARA, TUMBAKU

HOTUBA YA WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO, MHE. UMMY A. MWALIMU (MB), KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2018/2019

MADAI YA WAFANYAKAZI YASABABISHA VIFAA VYA UJENZI VYA KAMPUNI YA  CEYTUN KUZUIWA UWANJA WA NDEGE TABORA.