NI RAHISI SANA KWA SHETANI KUWA MTAKATIFU KULIKO MAGAZETI YOTE YALIYOPO KUTIMIZA VIGEZO VYA KUSAJILIWA UPYA


HUKU tarehe 15 Oktoba ikitangazwa kuwa ndio mwisho wa mchakato wa usajili wa magazeti yakiwamo yale ambayo yameshasajiliwa, kuna dalili za wazi huenda magazeti mengi yasisajilike kutokana na kushindwa kutimiza masharti. Mojawapo ya sharti gumu kuliko yote ni rekodi ya kodi; kwamba ili usajiliwe ni lazima uwe umemalizana na mabwana kodi yaani TRA; hapo ndio shughuli ilipo. Kwamba, TRA wanatakiwa wakupe cheti kinachoonyesha kwamba hawakudai kodi….yaani TAX CLEARANCE. LAKINI UKWELI UKOJE KWENYE VYOMBO VYA HABARI? Karibu vyombo vingi vinadaiwa kodi, achilia mbali kushindwa kuwalipa wafanyakazi inavyotakiwa ikiwamo baadhi kutolipa mishahara ya miaka zaidi ya mitano. Vipo vyombo vya habari ambavyo havijawalipa wafanyakazi mishahara kwa zaidi ya miaka na vingine miezi minane na hata chini ya hapo. KAMA HAWAWALIPI WANAISHIJE? Swali zito hili lakini kila mbuzi anakula kulingana na urefu wa Kamba yake…huenda wanaishi kwa miujiza kama Malaria alivyopata uja uzito bila kukutana na mwanaume; Maisha ni mipango. KWANI KUNA MASHARTI GANI MENGINE? Yapo masharti mengine lakini hayana shida, balaa liko kwenye TAX CLEARANCE tu….Masharti mengine ni pamoja na sifa za waandishi, hili halina shida maana waandishi tumekwenda shule nyakati hizi…WACHA KABISA. Tangaza nafasi za kazi za kusaka waandishi, utakuwa na wakati mgumu kuchagua maana wazuri ni wengi. YAANI BALAA ZITO NI TAX CLEARANCE tu hakina ya nani. Sifa nyinginezo zinazotakiwa kwenye kusajili gazeti ni uwezo wa kifedha, angalau uwe na fedha za kuchapa matoleo KUMI; hilo sio suala gumu bwana, KASHESHE NI TAX CLEARANCE tu!! MTIRIRIKO KAMILI WA KUSAJILI GAZETI 1. Unapaswa kuwa na hati ya usajili wa Kampuni itakayoendesha biashara hiyo ya Gazeti. (WENGI WATAPENYA) 2. CV's za Director wa Kampuni hiyo (WENGI WATAPENYA) 3. CV's za Editor wako na waandishi 10 (WENGI WATAPENYA) 4. Bank Statement ya A/C ya kampuni yako ikionyesha uwezo wako wa Mtaji (WENGI WATAPENYA, WABONGO SI HABA ANAWEZA KUWEKA HATA CHEKI HEWA HALAFU AKAPRINT, ATAKAVYOCHAPISHA GAZETI ATAJUA MWENYEWE NA MUNGU WAKE, LAKINI HILI HALINA SHIDA SANA) 5. Location ya ofisi (WENGI WATAPENYA; si unasema tu uko Manzese uwanja wa fisi nk hakuna shida jamani) 6. Printer wa Magazeti yako, hapa anaweza kuwa ni kampuni namba ((WENGI WATAPENYA;) 7. CHETI CHA KUONYESHA HUDAIWI KODI; TAX CLEARANCE (BALAA LIKO HAPA) 8. Baada ya kukamilisha kwa msajili wa Magazeti utakwenda Maktaba kuandikisha ambako utapata ISSN namba. (HII HAINA SHIDA, NI NAMBA TU YA UTAMBULISHO KWAMBA GAZETI LAKO NI NAMBA NGAPI, NI KAMA BAKODI FULANI) 9. Utaandikisha Posta (HUKO HAKUNA SHIDA) Huenda kukawa na taratibu nyingine ZINAZOWEZA KUHITAJIKA AU KUTOHITAJIKA KWA AJILI YA KUPATA USAJILI WA GAZETI NJE YA ORODHA NILIYOIELEZA JUU; ni vizuri ukatembelea Idara ya Habari na maelezo (Msajili wa Magazeti) hapo utapewa Fomu kwa ajili ya maelekezo ya usajili. KIMSINGI BIASHARA YA MAGAZETI NI NZJRI NA INA MAANA SANA KWA JAMII KAMA TU UTALITUMIA GAZETI HILO KWA MAMBO YA MAANA.

Comments

Tanzania

TAARIFA MBAYA KWA WAVUTAJI WA SIGARA, TUMBAKU

HOTUBA YA WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO, MHE. UMMY A. MWALIMU (MB), KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2018/2019

MADAI YA WAFANYAKAZI YASABABISHA VIFAA VYA UJENZI VYA KAMPUNI YA  CEYTUN KUZUIWA UWANJA WA NDEGE TABORA.