Profesa Safari asema Chadema hakina fedha, aomba msaada Ujerumani na EU kumtibu Lissu


Na Mwandishi wetu CHADEMA inaendelea na harakati za kutafuta njia za kumtibia Mbunge wake, Tundu Lissu anayepata matibabu Kenya. Mwanasiasa huyo inadaiwa alipigwa risasi tumboni na miguuni; hali yake imekuwa nzuri na wakati fulani kubadilika na kuwa mbaya. Kulingana na taarifa ya Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Profesa Abdalah Safari ni kwamba matibabu yake yanagharimu kiasi cha Sh 10 milioni kwa siku. Gharama hizi kwa mujibu wa Profesa Safari ni kubwa, lakini chama kimeapa kitafanya inachoweza ili matibabu yafanyike. “Kwa sababu ya ukweli kwamba matibabu haya ni gharama kubwa, tumeziomba jumuiya za kimataifa ikiwamo Ujerumani na Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU) kutusaidia matibabu”. Chama, kwa mujibu wa Profesa kimeunda kamati maalumu ya kuratibu michango na moja ya sehemu walizowasilisha maombi ni kwa Serikali ya Ujerumani na Umoja wa Ulaya. “Siwezi kusema hadi sasa nini tumejibiwa, lakini kamati inaendelea kufuatilia, Wajerumani ni ndugu zetu maana chama cha CDU ni marafiki zetu na tumewaandikia,” alisema. “Hatuna fedha, lazima tuendelee kutafuta njia nyingine za kumwokoa ndugu yetu,” alisema Profesa Safari.

Comments

Tanzania

HOTUBA YA WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO, MHE. UMMY A. MWALIMU (MB), KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2018/2019

Hatua za Ugonjwa wa UKIMWI

MAITI YAOKOTWA IKIWA KWENYE MFUKO, MIKONO NA MIGUU YAFUNGWA KAMBA KWA NYUMA