RC MWANRI AAGIZA MA-DC KULINDA RASILIMALI-MISITU KATIKA WILAYA ZAO


WAKUU wa wilaya wote katika mikoa ya Kigoma, Katavi, Tabora na Shinyanga wametakiwa kulinda na kusimamia ipasavyo rasilimali-misitu zilizoko katika wilaya zao ili  kunusuru vitendo vya uharibifu wa misitu vinavyofanywa na wananchi katika maeneo hayo. Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanry alipokuwa akifungua semina elekezi ya utekelezaji na usimamizi wa rasilimali-misitu iliyoko katika mikoa yote ya Kanda ya Magharibi iliyofanyika jana Mkoani hapa. Alisema wakuu wa wilaya ndio wasimamizi wakuu wa rasilimali zote za nchi katika wilaya zao hivyo wanatakiwa kuzisimamia ipasavyo ili kuepusha uharibifu mkubwa unaoendelea katika maeneo mbalimbali hapa nchini ikiwemo Kanda ya Magharibi. Alibainisha kuwa kama mikoa hiyo itashirikiana kwa ukaribu zaidi kuboresha usimamizi wa rasilimali zote zilizoko katika Kanda hiyo uoto wa asili utarudi katika hali yake ya kawaida misitu itachipua na mazingira kuboreshwa zaidi hivyo kuchochea upatikanaji wa mvua na kuimarisha kilimo ili kupunguza umasikini. ‘Haiingii akilini, DC upo, lakini miti inakatwa ovyo ovyo kila siku na kuchomwa kwa ajli ya shughuli za kibinadamu teana katika maeneo ya hifadhi, hili halikubaliki hata kidogo’, alisema. Mwanri alisema kama viongozi na watendaji wote wa halmashauri za wilaya hizo watakuwa na msimamo wa pamoja watafanikisha azma ya serikali ya kutokomeza vitendo vya uharibifu wa mazingira katika Kanda hiyo. Aliwataka kukemea kwa nguvu zao zote na kuwachukulia hatua wale wote wanaoendeleza vitendo vya ukataji miti ovyo na kuharibu misitu ili kulinda mazao ya misitu hiyo ambayo ni asali, mbao na oxygen. , hivyo misitu ni utalii misitu ni uhai basi tushirikiane tuitunze. Aidha aliongeza kuwa baadhi ya wananchi wamekuwa na tabia ya kuchoma mkaa na kuuza bila kibali hivyo akaagiza kukamatwa kwa yeyote atakayekutwa anasafirisha mkaa bila kibali ili hatua za kisheria zichukuliwe. Msimamizi Mkuu wa Misitu hapa nchini Ismail Aloo alisema hadi sasa takwimu zinaonesha zaidi ya hekta laki tatu za misitu zimeharibiwa kutokana na ukataji miti hovyo, kuhamahama kwa wakulima na wafugaji huku akibainisha kuwa mikoa ya Kanda hiyo inaongoza kwa kutokuwa na misitu. Alisema wananchi wanapaswa kuenenda na kauli isemayo kata mti panda mti na ikiwezekana ukikata mti mmoja panda miti mitatu hiyo itasaidia sana hata kukuza uchumi wa nchi kutokana na misitu

Comments

Tanzania

HOTUBA YA WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO, MHE. UMMY A. MWALIMU (MB), KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2018/2019

Hatua za Ugonjwa wa UKIMWI

MAITI YAOKOTWA IKIWA KWENYE MFUKO, MIKONO NA MIGUU YAFUNGWA KAMBA KWA NYUMA