YONO, TRA kupiga mnada magorofa ya Lugumi kesho


YONO, TRA kupiga mnada magorofa ya Lugumi kesho Na Mwandishi wetu KAMPUNI ya Udalali ya Yono Action Mart kesho inatarajia kuyapiga mnada majego ya kifahali ya Mfanyabiashara maarufu nchini Said Lugumi. Mnada huo utaendeshwa na kampuni ya Yono iliyopewa Mamlaka na Serikali chini ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutokana na kudaiwa mabilioni ya shilingi. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Slaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Udalali ya Yono,Scholastika Kevela, alisema nyumba hizo zinazopigwa mnada zipo Upanga na Mbweni. "Kwa idhini niliopewa na Serikali na TRA kampuni yangu inatarajia kuendesha mnada huo kesho watanzania wameombwa kujitokeza kununua majengo hayo ili fedha za kodi ya serikali ziweze kupatikana"alisema Kevela. Kevela alisema majengo hayo yalianza kushikiliwa na Serikali Mwezi April mwaka huu kutokana na kudaiwa deni kubwa na serikali. Alisema mfanyabiashara huyo, alikuwa na taarifa za kudaiwa deni hilo kubwa na serikali na zilifungwa kwa muda wote huo ili aweze kulipa kodi hiyo ya serikali. Sakata la Lugumi liliwasilishwa Bungeni mwaka jana, ambapo kutokana na mtifuano huo Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ilifanya uchunguzi kuhusu mkataba tata kati ya Jeshi la Polisi na Kampuni ya Lugumi Enteprises Limited . Kampuni ya Lugumi ilipewa Zabuni na Jeshi la polisi kwa ajili ya kufunga mashine za kuchukua alama za vidole katika vituo 108 nchi nzima kwa gharama ya shilingi bilioni 37. Hata hivyo mashine hizo zilifungwa katika vituo 14 vya polisi wakati kampuni hiyo imekwisha lipwa sh,bilioni 34 sawa na asilimia 99 ya fedha za mkataba.

Comments

Tanzania

TAARIFA MBAYA KWA WAVUTAJI WA SIGARA, TUMBAKU

HOTUBA YA WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO, MHE. UMMY A. MWALIMU (MB), KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2018/2019

MADAI YA WAFANYAKAZI YASABABISHA VIFAA VYA UJENZI VYA KAMPUNI YA  CEYTUN KUZUIWA UWANJA WA NDEGE TABORA.