Posts

Showing posts from October, 2017

Public Relations And Protocol Officer III

The Public Relations and Protocol Officer will organize and deliver key information to clients and stakeholders through electronic media. Job Description Position: Public Relations and Protocol Officer III -1 Post Reports to: Head of Division Contract type: Unspecified period Job Purpose: To organize and deliver key information to clients and stakeholders through electronic media. Key Performance Areas: a) Organise Bank’s engagement with the media. b) Manage, maintain and produce content for the Bank website, including multimedia content. c) Take photos (still and video) during Bank’s events and maintain photographic records. d) Manage, edit and produce content for the Bank’s social media platforms. e) Monitor and prepare responses to issues raised by the media/stakeholders. f) Participate in the organisation and preparation of various functions hosted by the Bank. g) Summarise news from local and foreign media on various key issues. h) Provide inputs for development and review of p…

ZAIDI YA WANAFUNZI 70 WANUSULIKA KIFO BAADA YA BWENI LAO KUTEKETEA KWA MOTO

People Stevie Chindiyesa To majira majira2006 majira2006 Today at 3:22 PM Na Mwandishi wetu, Tunduru ZAIDI ya Wanafunzi 70 wanao soma katika Shule ya Sekondari ya Nandembo Wilaysani Tunduru Mkoani Ruvuma wamenusulika kifo baada ya Bweni walimo kuwa wakilala kuteketea kwa moto. Taarifa za tukio hilo zinzeleza kuwa Sambamba na moto huo kutekeketeza bweni hilo pia moto huo uliunguza na kuteketeza, Madaftari, Nguo na mashuka pamoja na mali za wanafunzi waliokuwa wakilala humo na kuwaacha wakiwa na nguo walizo kuwa nazo katika miili yao. Mashuhuda wa tukio hilo walisema kuwa Bweni hili walilo kuwa wakilala Wanafunzi wa kiume wanaosoma kidato cha kwanza na kidato cha Nne lili lipuka moto Oktoba 16 mwaka huu majira ya kati ya saa 1.30 na saa 2. 00 za usiku. Akizungumzia tukio hilo Mkuu wa Shule hiyo Mwl. Mary Ndunguru alisema kuwa baada ta kuzuka kwa moto huo yeye, Walimu kwa kushirikiana na wanafunzi walijitahidi kuuzima moto huo bila mafanikio. Alisema wakati moto h…

SAKATA LA WABUNGE CUF MAALIM, LIPUMBA KUJULIKANA KESHO

Image
KESHO mbele ya Mheshimiwa Jaji Lugano Mwandambo imepangwa kutajwa Shauri la Msingi Namba 143/2017 kati ya Wabunge 8 na Madiwani 2 dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali-AG, Bunge, NEC, Halmashauri za UBungo na Temeke, pamoja na Lipumba na wenzake (8) litapangiwa utaratibu wa kusikilizwa Mapingamizi yaliyowekwa na Lipumba na Wenzake. Hili ndilo shauri la msingi linalohoji uhalali wa Lipumba na Baraza Kuu lake kuwavua uanachama Wabunge na Madiwani. .

AHUKUMIWA JELA MIAKA 20 KWA KUMVUA NGUO ZA NDANI MTOTO WA KIKE

Image
Na Mwandishi wetu MAHAKAMA ya Hakimu Mfawidhi wa wilaya ya Igunga mkoani Tabora imemhukumu Mtandi Nassoro (24) mkazi wa Igunga mjini kutumikia adhabu ya kifungo cha miaka 20 jela baada ya kupatikana na kosa la shambulio la aibu kwa mtoto wa miaka 5 ambaye jina lake limehifadhiwa. Mwendesha mashitaka wa Jeshi la Polisi Elmajid Kweyamba aliiambia mahakama mbele ya hakimu wa wilaya hiyo Ajali Milanzi kuwa mshitakiwa Mtandi Nassoro alitenda kosa hilo Mei 18 mwaka huu majira ya saa 4 asubuhi katika mtaa wa stoo mjini Igunga. Alifafanua kuwa mshtakiwa alimfanyia shambulio la aibu mtoto mdogo mwenye umri wa miaka 5 kwa kumvua nguo za ndani na kumshika shika sehemu za siri. Alisema mshitakiwa alitenda kosa hilo kinyume na kifungu 138 C (1)(a)(2)(b) sura ya 16 mapitio ya 2002 inayozuia kutenda makosa kama hayo. Baada ya kusomewa shitaka mshitakiwa alikana kutenda kosa hilo na ndipo upande wa Jamhuri ulipeleka mashahidi watano mahakamani akiwemo mtoto aliyeshambuliwa ambao wote walitoa …

WALENGWA WA TASAF WATAKIWA KUJIUNGA PAMOJA KUKABILIANA MAGONJWA YA KUKU.

Na Tiganya Vincent RS-Tabora 6 OKTOBA 2017 WALENGWA wa Mpango wa kunusuru kaya Maskini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii(TASAF) wametakiwa kuanzisha vikundi vya ufugaji kuku ili waweze kuunganisha nguvu zao kwa ajili ya kutafuta dawa za chanjo zitakazowasaidia kukabiliana na ugonjwa wa mdodo na kideri(Newcastle diasese) ambao umekuwa ukiwasababishia hasara. Kauli hiyo imetolewa jana na Mchumi Mkuu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora Richius Bilakwata kwenye mikutano na walengwa wa vijiji vya Itebulanda na Nsenda wilayani Urambo. Alisema kuwa ili waweze kuepuka kupata hasara kutokana na kuku zao kushambuliwa na ugonjwa huo ni vema wakawa wananunua chanjo na kuwachanja. “Moja ya chanjo inaweza kuchanja kuku wengi kwa pamoja ni vema mkajiunga pamoja ili muweze kuchangia katika ununuzi wa dawa hiyo kwa urahisi” alisema Bilakwata. Aliwashauri walengwa kuwa wakati mpango huu wa kunusuru kaya ukielekea mwishoni ni vema wakajitihidi kutumia kipato kidogo wanachokipata …