WALENGWA WA TASAF WATAKIWA KUJIUNGA PAMOJA KUKABILIANA MAGONJWA YA KUKU.


Na Tiganya Vincent RS-Tabora 6 OKTOBA 2017 WALENGWA wa Mpango wa kunusuru kaya Maskini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii(TASAF) wametakiwa kuanzisha vikundi vya ufugaji kuku ili waweze kuunganisha nguvu zao kwa ajili ya kutafuta dawa za chanjo zitakazowasaidia kukabiliana na ugonjwa wa mdodo na kideri(Newcastle diasese) ambao umekuwa ukiwasababishia hasara. Kauli hiyo imetolewa jana na Mchumi Mkuu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora Richius Bilakwata kwenye mikutano na walengwa wa vijiji vya Itebulanda na Nsenda wilayani Urambo. Alisema kuwa ili waweze kuepuka kupata hasara kutokana na kuku zao kushambuliwa na ugonjwa huo ni vema wakawa wananunua chanjo na kuwachanja. “Moja ya chanjo inaweza kuchanja kuku wengi kwa pamoja ni vema mkajiunga pamoja ili muweze kuchangia katika ununuzi wa dawa hiyo kwa urahisi” alisema Bilakwata. Aliwashauri walengwa kuwa wakati mpango huu wa kunusuru kaya ukielekea mwishoni ni vema wakajitihidi kutumia kipato kidogo wanachokipata kuwekeza katika miradi midogo kama vile ufugaji wa bata, kuku, mbuzi na mifugo mingine. Bilakwata alisema kuwa miradi hiyo itawasaidia wakati mpango huo utakapokuwa umekoma. Nao walengwa wengi walisema kuwa wamekata tama kuendelea na ufugaji wa kuku kwa sababu ya kushambuliwa na magonjwa kama vile mdodo na kideri. Hivi sasa kuku moja katika maeneo ya Urambo mjini anauzwa kwa wastani wa shilingi elfu 8 hadi elfu 12.

Comments

Tanzania

TAARIFA MBAYA KWA WAVUTAJI WA SIGARA, TUMBAKU

HOTUBA YA WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO, MHE. UMMY A. MWALIMU (MB), KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2018/2019

MADAI YA WAFANYAKAZI YASABABISHA VIFAA VYA UJENZI VYA KAMPUNI YA  CEYTUN KUZUIWA UWANJA WA NDEGE TABORA.