ZAIDI YA WANAFUNZI 70 WANUSULIKA KIFO BAADA YA BWENI LAO KUTEKETEA KWA MOTO


People Stevie Chindiyesa To majira majira2006 majira2006 Today at 3:22 PM Na Mwandishi wetu, Tunduru ZAIDI ya Wanafunzi 70 wanao soma katika Shule ya Sekondari ya Nandembo Wilaysani Tunduru Mkoani Ruvuma wamenusulika kifo baada ya Bweni walimo kuwa wakilala kuteketea kwa moto. Taarifa za tukio hilo zinzeleza kuwa Sambamba na moto huo kutekeketeza bweni hilo pia moto huo uliunguza na kuteketeza, Madaftari, Nguo na mashuka pamoja na mali za wanafunzi waliokuwa wakilala humo na kuwaacha wakiwa na nguo walizo kuwa nazo katika miili yao. Mashuhuda wa tukio hilo walisema kuwa Bweni hili walilo kuwa wakilala Wanafunzi wa kiume wanaosoma kidato cha kwanza na kidato cha Nne lili lipuka moto Oktoba 16 mwaka huu majira ya kati ya saa 1.30 na saa 2. 00 za usiku. Akizungumzia tukio hilo Mkuu wa Shule hiyo Mwl. Mary Ndunguru alisema kuwa baada ta kuzuka kwa moto huo yeye, Walimu kwa kushirikiana na wanafunzi walijitahidi kuuzima moto huo bila mafanikio. Alisema wakati moto huo ukiwaka katika bweni hilo wanafunzi wote walikuwa wakiendelea na masomo ya jioni katika madarasa yaliyopo umbali wa zaidi ya kita 200 jambo ambalo liliwafanya wachelewe kuubaini. Mwl. Ndunguru aliendelea kufafanua kuwa baada ya tukio la kuudhibiti moto huo kukamilika na kubaini kutokuwepo kwa uwezekeno wa wanafunzi kuendelea kulala katika bweni hilo aliwasiliana na Viongozi wa Kanisa Katoliki Kijijini hapo na kuwaombea wanafunzi hao ili waende kulala hapo kwa muda wakati Viongozi wa halmashauri hiyo wakiendelea na juhudi za kutafuta ufumbuzi wa kuwajengea Bweni jingine. Akizungumzia tukio hilo Kaimu afisa eliomu wa Shule za Sekondari Wilayani Tunduru, Mwl. Habiba Mfaume alisema kuwa takwimu zinaonesha kuwa jumla ya Wanafunzi 72 walikuwa wanalala katika Bweni hilo na kwamba hakuna mwanafunzi aliyepata madhara katika tukio hilo. Alisema kutokana na hali hiyo tayali amemuagiza Mkuu wa Shule hiyo kuwaita wazazi wote kushirika katika kikao kilicho pangwa kufanyika alhamisi ya Wiki hii ili kuomba msaada wa awali kwao na kwamba kila mzazi ajitahidi kufika na nguo zitakazo saidia kuwasitiri watoto wao katika kipindi hicho cha mpito. Naye kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Chiza Marando alisema kuwa ili kuwasaidia wanafuzni wanaojiandaa kufanya mitihani ya kuhitimu masomo ya kidato cha nne inayotarajiwa kuanza Oktoba 30 mwaka huu tayali amekwisha watuma wataalamu kupitia masomo yote waliyosoma ili waweze kuwasaidia kuwatolea nakala za photo copy wanafunzi wote zikiwa ni juhudi za kuwafanya waendelee kujisomea. Akiongea kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Tunduru ambye ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na usalama, kaimu afisa Tawala wa Wilaya hiyo, Agustino Maneno alisema kuwa tayali amekwishi muagiza kamanda wa Polisi wa Wilaya hiyo kupeleka wataalamu wa jeshi hilo kwa ajili ya kupeleleza chanzo cha moto huo. Mwisho

Comments

Tanzania

TAARIFA MBAYA KWA WAVUTAJI WA SIGARA, TUMBAKU

HOTUBA YA WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO, MHE. UMMY A. MWALIMU (MB), KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2018/2019

MADAI YA WAFANYAKAZI YASABABISHA VIFAA VYA UJENZI VYA KAMPUNI YA  CEYTUN KUZUIWA UWANJA WA NDEGE TABORA.