WAOMBA ADHABU Y A KIFO ITEKELEZWE


> Na Mwandishi wetu,Rukwa > BAADHI ya wakazi mkoani Rukwa wamemuomba Rais John Magufuli abadili msimamo wake na kuanza kuidhinisha wafungwa waliohukumiwa kunyongwa,wanyongwe ili kupunguza mauaji holela ya watu wasio na hatia yanayoendelea kutokea. > > Ombi hilo limetolewa jana kwa nyakati tofauti baada ya kutokea mauaji ya Telestina Silanda(45) mkazi wa kijiji cha China kata ya Kate wilayani Nkasi baada ya kuuawa kwa kuchinjwa na watu Wasiojulikana akiwanyumbani kwake. > > mmoja wa wakazi wa mjini Sumbawanga mkoani humo aliyejitambulisha kwa jina la Frank Paschal alisema kuwa kutokana na kuwa adhabu ya kunyonga haijatekelezwa muda mrefu hapa nchini huenda ikawa ni sababu ya baadhi ya watu kufanya mauaji holela kwakua wanajua hata wakiua hawata nyongwa watakwenda kukaa gerezani kwa maisha yao yote. > > Alisema kuwa kumbukumbu zinaonesha kuwa adhabu hiyo ilitekelezwa kwa rais wa awamu ya pili lakini marais waliofuata wamekuwa wakikwepa kuidhinisha watu waliohukumiwa kunyongwa,wanyongwe huenda ikawa ni sababu ya kuongezeka kwa mauaji holela ikiwemo ya vikongwe,albino na wanaotuhumiwa kwa ushirikina. > > Paschal alisema kuwa hivi sasa watu hawana hofu tena ya kufanya mauaji kwa kulipizana visasi ama tamaa ya kujipatia mali hali ambayo inazidi kuota mizizi katika jamii kutokana na kutotekelezwa hukumu ya kunyonga kwa muda mrefu. > > Naye Janeth Kapama mkazi wa wilaya ya Nkasi mkoani humo alisema kuwa kwakua sheria hiyo bado ipo na haijafutwa ni vizuri raisi akaitekeleza huenda itasaidia kuleta hofu na kupunguza tabia ya baadhi ya watu kufanya mauaji holela. > > "hivi vitendo vya viongozi wa nchi kutoridhia waliohukumiwa kunyongwa,wanyongwe kunachangia kuendelea kwa mauaji holela,kama hawataki basi sheria ifutwe kuliko kuwa nayo halafu haifanyiwi kazi" alisema > > Alisema kumekuwa na kushamili kwa mauaji holela katika sehemu mbalimbali tena ukifuatilia unakuta ni kwasababu zisizo na msingi kama kuzushiwa ushirikina,tamaa ya mali na wivu wa maendeleo yote ni kutokana na kuwa wauaji hawanyongwi ndiyo maana baadhi yao wamekuwa hawaogopi kuwaua wenzao. > > Alimuomba rais Magufuli kusaini kutekelezwa kwa hukumu hiyo kwa nia njema ili kukomesha mauaji hayo tofauti na hivyo itakua ngumu kudhibiti mauaji holela kwani kitendo cha kuogopa kinasababisha baadhi ya wa watu waendelee kuwaua wenzao kikatili. > > "Tunajua rais wetu yupo makini katika kusimamia sheria za nchi kwani tumekuwa tukimuona ni msaada mkubwa kwa wanaoporwa viwanja,kubomoa wanaokiuka sheria za ujenzi na sheria nyingine nyinyi hivyo hapaswi kuogopa hii ya kuidhinisha wauaji kunyongwa kwani atakuwa anasimamia utawala wa sheria na si vinginevyo"alisema > > Hata hivyo rais John Magufuli wakati akimuapisha jaji mkuu wa Tanzania alisema kuwa wasimpelekee mafaili ya watu walio hukumiwa kunyongwa kwani yeye binafsi hayupo tayari kuidhinisha watu hao wanyongwe. > > Mwisho

Comments

Tanzania

TAARIFA MBAYA KWA WAVUTAJI WA SIGARA, TUMBAKU

HOTUBA YA WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO, MHE. UMMY A. MWALIMU (MB), KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2018/2019

MADAI YA WAFANYAKAZI YASABABISHA VIFAA VYA UJENZI VYA KAMPUNI YA  CEYTUN KUZUIWA UWANJA WA NDEGE TABORA.