Posts

Showing posts from February, 2018

Unataka maisha bora, mwoga wa kujaribu

Na Dismas Lyassa HUWEZI kufanikiwa kama huthubutu kufanya mambo fulani. Kusoma sana au kidogo, kuwa na rafiki waliofanikiwa au wasiofanikiwa, kwenda nje ya nchi au la, au kuzaliwa familia maskini au tajiri, bado sio tiketi ya kukufanya uwe na maisha bora. Msingi wa kufanikiwa ni kuthubutu kufanya jambo fulani, kwa mfano kufungua mradi na mambo mengine kama haya. Kuna watu kwa mfano unaweza kuona anakata tamaa kwa sababu labda amezaliwa katika familia maskini, kitu ambacho sio sahihi. Msingi wa kuwa na maisha bora ni kufanya kazi kwa bidii na zaidi ni kuishi kwa malengo. Usiishi tu ili mradi siku zinakwenda mbele, ishi kwa malengo. Kwa chochote unachokifanya, kifanye baada ya kutafakari na kuangalia faida au hasara yake. Maisha yanatuhitaji kuwa waangalifu na wanadamu wanaotunguka, kwa sababu walio wengi furaha yao ni kuona unakuwa hauna mafanikio. Kuna wengine kwa mfano kabla ya kufanikiwa anakuwa ni rafiki, lakini ukishafanikiwa, anakuwa mtu mbaya. Kuna mwingine hata ukimwangalia …