Posts

Showing posts from April, 2018

HOTUBA YA WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO, MHE. UMMY A. MWALIMU (MB), KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2018/2019

Image
A: UTANGULIZI 1. Mheshimiwa Spika, kufuatia taarifa iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii ndani ya Bunge lako Tukufu, ambayo imechambua Bajeti ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, ninaomba kutoa hoja ili Bunge lako likubali kupokea na kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Kazi za Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa mwaka 2017/18 na Vipaumbele vya Wizara kwa mwaka 2018/19. Aidha, ninaliomba Bunge lako Tukufu likubali kupitisha Makadirio na Mapato ya Matumizi ya Kawaida pamoja na Mpango wa Maendeleo ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa mwaka 2018/19. 2. Mheshimiwa Spika, kwanza napenda kumshukuru Mwenyenzi Mungu kwa kuniwezesha kusimama mbele ya Bunge lako Tukufu na kuwasilisha hotuba yangu siku ya leo. Aidha, ninapenda kutumia fursa hii kwa heshima na unyenyekevu mkubwa kumshukuru kwa dhati Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muun…